Habari

Mahakama ya hakimu mkazi yawaondolea zuio viongozi wa EAGT

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jumanne Januari 9, imefuta amri ya kumzuia kwa muda Askofu Mkuu wa Kanisa la The Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk Brown Mwakipesile na wenzake, kujishughulisha na mambo ya kanisa hilo kwa nafasi zao, ikiwemo kufanya miamala kwenye akaunti ya kanisa.

Amri hiyo ilitolewa na mahakama hiyo Desemba 21, mwaka jana kufuatia maombi ya mlalamikaji aliyejitambulisha mahakamani hapo kuwa ni Bodi ya Wadhamini wa kanisa hilo. Amri hiyo ilitolewa bila uwepo wa wakili wala walalamikiwa wote, ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, mchungaji Dk Leonard Mwizarubi, na mweka Hazina, mchungaji Praygod Mgonja.

Pamoja na kufuta amri hiyo, Mahakama hiyo pia imewataka wachungaji waliochaguliwa kuwa viongozi mbadala wa kanisa hilo katika uchaguzi uliofanyika katika mkutano ulioitishwa na mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa kanisa hilo Mchungaji John Mfuko na kufanyika Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam, kuacha mara moja kufanya shughuli za uongozi wa EAGT na wakikaidi wakamatwe mara moja.

Uamuzi huo ulifikiwa na mahakama kabla hata ya kusikilizwa kwa mapingamizi kutoka kwa mawakili wa wadaiwa baada ya wakili wa wadai, Bahati Mabula kushindwa kutokea mahakamani na sababu za kutokuwepo kwake kukosa mashiko. Wakati mahakama inafikia uamuzi huo mchungaji Mfuko, ambaye ndiye mlalamikaji kwa nafasi yake ya uenyekiti wa bodi alikuwepo mahakamani hapo. Mapingamizi hayo sasa yatasikilizwa Januri 19, mwaka huu.

Mahakama iliridhika na hoja zilizowasilishwa na wakili wa wadaiwa Didace Kanyambo, ikiwemo kwamba uharaka waliokuwa nao wadai wakati wakiomba kwa hati ya dharura kuwazuia viongozi wa EAGT kujishughulisha na kazi za kanisa kwa nafasi zao, wameshindwa kuuthibitisha mahakama kutokana na wakili Mabula kuonyesha dhahiri tangu awali kuwa alitaka kutumia amri ya mahakama kusinzia huku shughuli za kanisa, ambayo ni taasisi yenye watu zaidi ya milioni 5 zikisimama.

Ili kusoma kwa undani zaidi kilichojiri mahakamani pamoja na mambo mengine kuhusu sakata hili, usikose kusoma gazeti la Kikristo la mtandaoni la Mwanzo Jumapili wiki hii. Gazeti hilo hupatikana katika tovuti ya mwanzonews.com au unaweza kuwasiliana nao kwa simu 0784942443 au 0754649941

Chanzo: mwanzo news

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video: Benachi - Tiba Yangu

Next post

Video | Audio: Sunny Praise – You Are Beautiful