Audio: Zile - Wela - Gospo Media
Connect with us

Audio: Zile – Wela

Audio

Audio: Zile – Wela

Kutoka nchini zambia leo nimekusogezea wimbo uitwao Wela kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Zile.

Zile ni mwimbaji na mtunzi ambaye ana shauku ya kutumika katika muziki ili kukomboa nafsi zilizopotea na zilizovunjika. Yeye pia ni mpigaji mzuri wa gitaa ya acoustic. Mbali na kuwa mwimbaji binafsi yeye pia ni mmoja wa wanamuziki wa bendi ya Jazz inayoitwa soul light on the copperbelt.

Zile pia ni mjasiriamali mdogo na alianza kuwa na shauku ya kufanya muziki tangu alipokuwa na umri wa miaka 17. Ana hamu ya kuwawezesha vijana wenzake kiroho na kuwasaidia kutambua vipaji vyao. Amebeba matumaini ya kutumia muziki wake kama jukwaa la kuathiri kizazi cha sasa katika kuleta uponyaji kwa mioyo iliyovunjika na kukata tamaa kupitia jina la Yesu Kristo.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu, Barikiwa.

 

Download Audio

Unaweza kusaidia Gospo Media kwa kuchangia chochote utakachoguswa ili tuzidi kuieneza Injili duniani kote,
M-PESA +255 755 038 159. Barikiwa

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top