Connect with us

Audio: Zephania Nanyaro – Baraka

Muziki

Audio: Zephania Nanyaro – Baraka

Kutoka Tarangire mkoani Manyara leo kwa mara ya kwanza nimekuletea wimbo uitwao Baraka kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akifahamika kwa jina la Zephania Nanyaro. Muziki huu umetayarishwa na mikono ya prodyuza Robyson Nnko na kurekodiwa ndani ya studio za K.M.P Records zilizopo mjini Karatu.

“Baraka” ni wimbo uliobeba maombi ya shukrani na ujazo wa Baraka kutoka kwa Mungu kuingia katika maisha yetu kwa maana aliahidi baraka nyingi katika maisha yetu nasi tuna tumaini kuwa Bwana Yesu atafanya haijalishi tutasubiri kwa muda gani, lakini tumaini letu bado lipo kwake kuwa ipo siku tutabarikiwa kwa maana ahadi zake ni za kweli.

“Huu wimbo unahusu ahadi alizotuahidi Mungu japo kila mmoja anafahamu ana ahadi gani kwa Mungu. Pia huu ni wimbo unaotia moyo katika kusubiri hata ikiwa imechelewa, pia katika yote atakayotenda ni lazima kushukuru na kuwa mvumilivu katika kuwa na tumaini kwa Mungu aliyehai.” – alisema Zephania.

Mwanzo 49:25 “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.

Baraka ni wimbo unaobeba jina la albamu yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni, Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu uliobeba tumaini lako juu ya Baraka za Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Zephania Nanyaro kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 7 53 51 84 78 au +255 659 244 272
Facebook: Zepha Nanyaro
Instagram: @zephananyaro
E-mail: zehaniananyaro@gmail.com
Youtube: Zephania Nanyaro

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top