Zaidi ya Majengo Elfu Moja ya Ibada Yamefungwa Nchini Angola - Gospo Media
Connect with us

Zaidi ya Majengo Elfu Moja ya Ibada Yamefungwa Nchini Angola

Habari

Zaidi ya Majengo Elfu Moja ya Ibada Yamefungwa Nchini Angola

Catholic-church-in-Angola

Zaidi ya majengo elfu moja ya ibada za kikristo yalifungwa na mamlaka nchini Angola kati ya tarehe 6 Novemba hadi 25 Desemba 2018 kutokana kuibuka kwa dini nyingi kila kukicha bila mpangilio na bila kuwa na kibali.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukubaliwa kwa mswada mpya wa sheria na kupitishwa ambapo unataka kila aina ya dhehebu ya dini kujiandikisha serikalini na kupata kibali pia angalau waamini wa dhehebu hilo wafikie laki moja.

Kila kikundi cha dini lazima kijiandikishe katika ofisi ya Waziri wa Haki na Utamaduni, japokuwa kabla ya sheria hiyo kupitishwa baadhi ya makanisa hayo yalikuwa tayari  yako nje ya sheria kwa mujibu wa Mkutano wa Mawaziri wa Angola kabla ya kuchukua hatua hiyo kwa ajili ya mchakato wa uundaji na marekebisho ya kufunga majengo hayo.

Taarifa inasema sheria mpya ya sasa nchini Angola inahitaji dini zote zijiorodheshe katika Ofisi ya waziri wa Haki na Utamaduni ili  kupata kibali cha haki ya utambulisho wa huduma za ibada. Lengo la kujiandikisha ni pamoja na kuthibiti majengo ambayo yamekuwa hayastahiki kwa mujibu wa sheria mpya, Na zaidi Kanisa hilo liwe na waamini angalau laki moja katika wilaya 12 kati ya wilaya 18 za nchi ya Angola.

Kwa kufuatia vigezo hivyo ni wazi kwamba kuna uthibiti au hakuna ruhusa ya makundi madogo madogo mapya ya kidini yanaweza kujiandikisha ili kupata kibali kama vile makundi yanayoibuka ya kiinjili na kiislam nchini Angola.

Chanzo: Vatican News

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top