Connect with us

Audio Music: Yz Manamba – Nasubiri

Muziki

Audio Music: Yz Manamba – Nasubiri

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa mara nyingine tena nimekuletea wimbo mzuri wenye kutia moyo uitwao Nasubiri kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayezidi kufanya vizuri katika kianda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la YZ Manamba, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Masai Records chini ya mikono ya prodyuza George Emil.

Nasubiri ni wimbo wa uliobeba ujumbe wa matumaini na faraja kwa wana Mungu ambao kwasasa wamekuwa na roho ya kukata tamaa kutokana na vikwazo na changamoto ambazo kwa namna moja ama nyingine ziawarudisha nyuma katika Imani, hivyo kupitia wimbo huu mwimbaji Yz Manamba anatukumbusha juu ya kuwa na uvumilivu ndani ya Yesu Kristo ili aweze kutenda miujiza ya baraka ndani ya maisha yetu.

Maisha leo yamekuwa na changamoto nyingi sana ambazo zinaweza kupelekea kukuweka mbali na uso wa Mungu lakini neno linasema ”Mtegemee Mwenyezi Mungu! Uwe na moyo, usikate tamaa! Naam, mtegemee Mwenyezi-Mungu!” – Zaburi 27:14

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao utakwenda kujaza tumaini jipya na kukupa nguvu mpya ya kumtumainia Mungu katika roho na kweli kwakuwa kwake hakuna linaloshindikana. Karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji YZ Manamba kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 747 350
Facebook: Yz Manamba Zacharia
Instagram: @yz_manambatz

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top