Video

Video | Audio: Yz Manamba – Ameniona

Baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake uitwao ”Nasubiri” aliouachia mwishoni mwa mwaka 2017 kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 mwimbaji Yz Manamba ametuletea video yake nzuri na yenye kutia moyo na kubariki iitwayo Ameniona, video hii imeongozwa na Director Robert na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Masai Records chini ya mikono ya prodyuza George Emil.

Ameniona ni wimbo uliojaa sifa na kubeba ujumbe wa matumaini kwa wana wa Mungu na kutoa msisitizo juu ya kumwamini Mungu kwakuwa kila tulifanyalo yeye huliona na kwa uweza wake hushusha baraka kwetu kwa yale ambayo tumefanya kwa utukufu wake.

”Hawezi kuuacha mguu wangu usogezwe, Hawezi kusinzia wakati wa magumu yangu, mi najua natembea nuruni mwake, hata hivi navyoimba Ananiona, Yeye ni mwema.” – Yz Manamba

Nina imani kuwa utabarikiwa kila utakapokuwa unatazama video hii na kupakua wimbo huu na hakika Mungu atakuona, Bwana atakuona, Ameen!.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Yz Manamba kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 747 350
Facebook: Yz Manamba Zacharia
Instagram: @yz_manambatz
Youtube: Yuzoh Manamba

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Mireille Basirwa - Holy Adonai

Next post

Audio: Rose Francis Feat. Eliud Martine – Nimeridhika Yesu