Video

Video | Audio: Yohana Mpangule – Nibariki

Kutoka jijini Dar es salaam leo nimekusogezea video iitwayo Nibariki kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Yohana Mpangule, video ya wimbo huu imeongozwa na Jogoo Film na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Flexible Entertainment.

Nibariki ni wimbo na video inayobeba jina la albamu yake mpya ambayo kwasasa ipo tayari akiwa bado anatafuta msambazaji, akizungumza na gospomedia.com kuhusiana na ujumbe ulio katika wimbo huu mwimbaji Yohana alisema:-

”Ujumbe ulio katika wimbo huu ni wa kumshukuru Mungu kwa NEEMA ya wokovu katika maisha yangu, ni hakika ameniokoa na mauti na sasa niko huru sina hofu ya mauti tena. Kweli Mungu amenitoa mbali sana, kwenye giza, upofu na kifungo akanipa Neema ya uhai, Nakuomba ungana nami katika maombi haya ya baraka za kiroho, tupate kumjua Mungu zaidi na zaidi siku hadi siku, Ameen.” – Alisema mtumishi Yohana Mpangule.

Nina Imani kuwa utabarikiwa kila utakapokuwa unatazama video hii na kusikiliza wimbo huu.. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi juu kuipata nakala ya albamu yake ya Nibariki na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Yohana Mpangule kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 762 839 003 au +255 713 839 003
Facebook: Yohana Mpangule
Instagram: @yohana_mpangule
Youtube: Yohana Mpangule

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Dona Jr. feat. Rebecca - Narudi

Next post

Audio: Joel Masingisa - Wastahili (You Deserve)