Uncategorized

Yajue Makosa Saba Ambayo Waimbaji Wa Muziki Wa Injili Hufanya Kwenye Biashara Ya Muziki.

1.KUISHI NYUMA YA MUDA KATIKA ULIMWENGU AMBAO HAUKUWA NA MITANDAO YA KIJAMII
Ujio wa mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter umerahisisha mawasiliano kwa kiasi kikubwa. Imerahisisha mawasiliano kati ya wasanii waimbaji na mashabiki wao au wasanii waimbaji na vyombo vya habari.
Bahati mbaya ni kwamba kuna wasanii wengi wenye allergy na mitandao ya kijamii. Haijulikani wako wapi, wanafanya nini, wanatoa lini wimbo mpya na kwa ufupi ni kwamba wamejichimbia shimoni. Kama haupo Facebook, Instagram wala Twitter, unategemea jina lako liongelewe wapi au huduma yako watu waipate vipi bila taarifa?social media

2.KUANIKA KILA KITU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Hakuna haja ya kuandika kwenye Twitter au Facebook kuhusu promoter wa Kahama aliyeshindwa kukulipa hela yako ya show na ukakosa nauli ya kurudi Dar es Salaam. Haikusaidii chochote zaidi ya kukushusha.
Blogs zitasherehekea kwakuwa zitakuwa zimepata habari nzuri ya kuvuta traffics na kukuchoresha zaidi wewe kwa vichwa vya habari. Wewe ni staa unayeishi ndoto zako basi itunze ndoto hiyo. Usimwambie kila mtu jinsi ulivyopigika na kwamba bado unaishi na mama yako ama kitu chochote kinachoweza kuharibu heshima kwa mashabiki wako. Kumbuka hauuzi tu muziki wako bali pia unauza wasifu wako.fb

3.KUPENDA KUPONDA WASANII WENZAKO/VYOMBO VYA HABARI/ WADAU WENGINE HADHARANI
Kuna wasanii wanaojiona wao ndio kila kitu. Wao ndio kikundi ama waimbaji bora tangu ulimwengu uanze. Maranyingi tumesikia wasanii ama waimbaji wakihojiwa redioni na kuanza kuponda nyimbo za watu wengine kana kwamba nyimbo zao zimetungwa kwa msaada wa malaika. Japokuwa una haki ya kutoa maoni yako pia unapaswa kukumbuka kuwa suala la kukosoa nyimbo hadharani ni kazi ya wachambuzi wasiofungamana na upande wowote. Unapokosoa wimbo wa mwenzio tambua kuwa kuna mashabiki wengi wanaoumpenda na kwa namna yoyote utakuwa umewakera pia. Hii tabia wanayo waimbaji wakongwe ambao wameprove failure na wanataka kuangushia lawama kwa wasanii wengine.HATERS

4. KUTOKUWA RAFIKI WA VYOMBO VYA HABARI
Ni ngumu kuwa karibu na redio, TV, magazeti ama blogs zote nchini lakini ni muhimu kuziheshimu zote. Ukiombwa interview na kituo cha radio cha Ludewa, unapaswa kuwa na muitikio sawa na kama unapoombwa interview na radio kubwa ya Dar es Salaam. Unapokuwa msanii ama muimbaji mkubwa, tambua kuwa kila kona ya nchi kuna mashabiki wako, hivyo usiwanyime fursa mashabiki wako wa vijijini kujua habari zako.preees

5.KUACHIA NYIMBO KWA MFUMO WA EXCLUSIVE
Media zote tunatakiwa kuzipa kipaumbele unapotaka kuachia nyimbo au video yako

6.KUWA NA MENEJA MBUMBUMBU
Asilima kubwa ya wasanii, waimbaji hasa wachanga wapo chini ya mameneja ama wasimamizi wenye pesa lakini wasio na ufahamu wa namna muziki wa Tanzania ulivyo. Wengi humsaidia msanii kwa kipindi fulani akitegemea matunda yaanze kuonekana ndani ya miezi mitatu. Kwa mazingira ya muziki ulivyo Tanzania ni ndoto kupata mafanikio katika kipindi hicho. Ni bora kuwa na meneja mwenye kipato cha kawaida lakini anayezijua njia na changamoto za muziki wa Tanzania, kuliko kuwa na meneja.

7.KUFULULIZA KUTOA NYIMBO ZINAZOFANANA
Kuna kichaa mmoja alipita sehemu na kuokota noti ya shilingi elfu moja. Basi kuanzia siku hiyo, alihakikisha
anapita eneo hilo zaidi ya mara 20 akitegemea kuwa ataokota tena hela nyingine. Huo ni mfano wa namna ya baadhi ya wasanii ama waimbaji wa Tanzania walivyo. Wimbo mmoja ukiwa hit, basi atahakikisha zingine mbili mpya zitakuwa ama na beat inayofanana na ya mwanzo ama ujumbe/mashairi sawa na wa mwanzo. Kwa mfumo huo, ni ndoto kufululiza kutoa hits bali utakuwa kama unaachia series.boredom
©Baba Kelly
Imeandaliwa na Baba Kelly na Zacky Maduhu, 0717 903 959

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

DOWNLOAD MUSIC AUDIO: NASHUKURU - GREGORY BERTAM MTENGA

Rungu la YEsu
Next post

MFAHAMU RUNGU LA YESU NA ALIVYOPAMBANA KWENYE MUZIKI WA GOSPEL HIP HOP TANZANIA.