Habari

Xclusive:Baada ya Ndoa,mtoto na mapumziko..Mwimbaji Neema Lyimo wa Mg’ong’o kurudi tena ulingoni.Sikiza wimbo wake mpya akimpa Mungu Shukurani.

Baada ya kutamba na wimbo wake wa TUVUKE NG’AMBO ,kweli dada yetu akavuka ng’ambo na hatimaye Mungu akamzawadia zawadi ya Mume na mtoto mmoja,na hapo ndipo mambo yakabadilika maana sio Neema Lyimo Yule tuliyemjua bali sasa ni Neema Lyimo wa Mng’ong’o ambapo sasa baada ya kula bata kidogo za maisha ya ndoa na mishe mishe za uzazi na malezi sasa dada yetu yuko fiti kurejea kwenye ulingo wa kupelekea Injili mbele kwa ile karama yake Mungu aliyompa.
Neema Lyimo wa Mng’ong’o ,mwanadada mwenye kiu ya kumtumikia Mungu anasema kwamba,” kama unahuduma ya Mungu popote pale, Mkutano wa Injili, Semina, Ibada nk, tushirikiane wala usiogope kunialika ili tujenge pamoja ufalme wa Kristo. Mambo ya fedha na gharama usiyafikilie kwanza, Mungu alinipa kazi na huduma hii bure kabisa, jambo la kwanza tumtumikie Mungu kwa urahisi ili kuujenga ufalme wa Mungu mengine Mungu atatupatia kwa wingi na kwa jinsi anayoijua yeye.”
Unaweza kumcheki dada Neema kupitia

Namba +255 753 777 057
E-mail: neemamngongo01@gmail.com
Facebook: Naitwa Neema Lyimo wa Mng’ong’o.
SikiliZa wimbo wake mpya unaitwa shukrani zangu.

https://soundcloud.com/sirmbezi-aloyce/neema-lyimo_shukuran-zangu

Advertisements
Previous post

Newz: Je wewe ni Muimbaji wa Nyimbo za Injili,Martha Mwaipaja anakupa fursaa hii hapa...

Next post

Gospo Audio Song: Rehema Sanga - Uitwe Mungu.