BurudaniHabari

Witness Mbise Kuzindua Nimegusa Vazi,May 14 CAG Ubungo Maziwa.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Witness Mbise yuko mbioni kuzindua album yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la NIMEGUSA VAZI.

Uzinduzi huo utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 14 May 2017 katika kanisa la CAG Ubungo Maziwa kwa Mchungaji Imelda Maboya kuanzia saa nane Mchana na kuendelea huku akisindikizwa na waimbaji mahiri kama vile Atosha Kissava,Upendo Nkone,Faraja Ntaboba,Beatrice Mwaipaja,Ritha Komba,Philipo Rupia na Wengine Wengi.

Akiongea na Gospomedia Witness amesema kuwa amejipanga kuhakikisha kuwa watu wote watakaohudhuria kwenye Uzinduzi wa Album yake hiyo Watabarikiwa vya kutosha.

Kwa kweli nimejipanga kimwili na kiroho kuhakikisha Mungu anaonekana kwenye uzinduzi wangu,kwa hiyo watu wasitarajie kumwona Witness peke yake bali watakutana na Mungu aliye hai” Alisema Witness Mbise.

Mwisho Witness Mbise amewaomba wadau wa Muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi kumtia moyo kwenye uzinduzi wake.Kumbuka Hakuna Kiingilio chochote kwenye Uzinduzi huu.

Advertisements
Previous post

Mkesha Wa Maombi Na Maombezi FPCT Chamwino Dodoma

Next post

Comedian Frank Mathew Anakuletea Laugh Again Concert Mei Mosi Ndani ya NIT