Connect with us

Audio: Witness Mbise – Baba ni Kichwa

Audio

Audio: Witness Mbise – Baba ni Kichwa

Baada ya kimya cha muda wa takribani mwaka mmoja mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Maarufu kama Witness Mbise kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia wimbo wake mpya uitwao Baba ni Kichwa.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Perfect Light chini ya mikono ya prodyuza Eric Madaraka.

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunifunulia siri hii ambayo ilikua imejificha na kufanya wengi wetu tukosee Sana. Na baada ya kuijua hii siri ndipo nilipata wazo la kuandika wimbo wa BABA NI KICHWA.

Siri yenyewe ni kuwa kumbe kumuheshimu Baba tunakua tumemheshimu Mungu moja kwa moja, Kwa maana tunakua tumeheshimu ule muda alitumia kumuumba huyu Baba. Niliangalia umuhimu wa mama ulivyo mkubwa na kwamba hili halipingiki kwa usemi tuliozoea kuwa “Hakuna Kama mama ” Ndio ni kweli lakini bado nafasi ya Baba ipo na iheshimiwe. Kuna mambo mazuri na makubwa yatendwayo na Baba zetu na nawahamasisha watu wamuheshim na kumlinda kwa maombi.” – alisema Witness

Tunaamini kupitia wimbo huu kuna jambo la kujifunza na hakika utabarikiwa kila wakati utakapokuwa unausikiliza, Ameen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Witness Mbise kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 676 631 067
Facebook: Witness Mbise
Instagram: @witnessmbiseofficial
Youtube: Witness Mbise

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top