Habari

Wanandoa wa kimisionari wafariki kwa ajali ya gari nchini Kongo

Na Mwandishi wetu,

Wanandoa wa kimisionari raia wa Marekani wamekutwa wamekufa katika ajali ya gari kusini mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wamisionari hao wa kibatist Randy na Kathy Arnett kutoka mji wa Missouri nchini marekani ambao walikuwa wakifanya kazi katika taasisi ya huduma ya kiroho iitwayo Congo4Christ walipatwa na ajali hiyo hiyi karibuni walipokuwa njiani kulekea kutoa mafunzo.

Kwa mujibu wa The Alabama Baptist taarifa zinasema kuwa wamisionari wengine wawili walijeruhiwa katika ajali hiyo akiwemo Jeff na Barbara Singerman, pamoja na rafiki yao mwenye asili ya kongo Jean Louis na dereva wao ambaye pia ni raia wa Kongo.

Kupitia ukurasa wa Facebook wa huduma ya Congo4Christ walitoa ujumbe wa kuomba watu maombi kwa familia zote zinazohusika, hasa kwa watoto wa mmsionari Arnetts wakati wakiendelea kupanga juu ya kuirejesha miili yao nchini Marekani.

Jeff na Barbara Singerman wamepelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya upasuaji.

Jeff na Barbara Singerman wamepelekwa mjini Johannesburg huko Afrika Kusini ili kupata matibabu kwa ajili ya majeraha yao, ambayo yanaelezwa kuwa ni makubwa yanayohitaji upasuaji.

Randy na Kathy Arnett walifanya kazi nchini Togo, Afrika Magharibi, na baadae katika nchi ya Ivory Coast. Randy alikuwa kiongozi wa kikanda wa IMB(International Mission Board) kwa Afrika Magharibi tangu mwaka 2004.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Askofu Mbepera azikwa kanisani kwake EAGT Galilaya

Next post

Video | Audio: Waba Shadra - Neno Moja