Video

Video | Audio: Walter Chilambo – Only You

Baada ya kuachia video yake iitwayo “Kuna Jambo” mwezi Novemba 2017 mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania Walter Chilambo ameachia video ya wimbo wake mpya iitwayo Only You ikiwa ni kazi yake ya kwanza kabisa katika mwaka 2018. Video hii imeongozwa na kampuni ya Perfect Light Studios zilizopo jijini Dar es salaam.

“Only You” ni wimbo uliobeba maombi ya kumshukuru Mungu kutoka kwa mtu ambaye anamtafakari Mungu katika kiwango cha juu kwa yale ambayo amemtendea katika maisha yake, Wimbo huu unamsihi Bwana Yesu aendelee kuwa msaada wa karibu katika mapito na hali zote tunazopitia katika maisha yetu sisi watoto wake.

Ni hakika kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu ambao nina imani kubwa kuwa utakubariki na kuinua nafsi yako hasa pale inapochoka na kukata tamaa, kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu, Mungu azidi kuwa egemeo na msaada pekee katika maisha yako, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Walter Chilambo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 718 069 509
Facebook: Walter Chilambo
Instagram: @walterchilambotz
Twittter: @walterchilambo
Youtube: Walter Chilambo

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Jahdiel – Winning

Next post

Video | Audio: Christopher Mwahangila & Bella D - Umenitoa Mbali