Audio: Walter Chilambo - Merry Christmas (Amezaliwa) - Gospo Media
Connect with us

Audio: Walter Chilambo – Merry Christmas (Amezaliwa)

Audio

Audio: Walter Chilambo – Merry Christmas (Amezaliwa)

Kutoka jijini Dar es salaam Tanzania leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tunautambulisha kwako wimbo mpya unaoitwa Merry Christmas(Amezaliwa) kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili anayejulikana kwa jina la Walter Chilambo wimbo huu umetengenezwa ndani ya studio ya Enzi Records chini ya mikono ya producer Amzy aliyeopo jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com Walter amesema kuwa ametoa zawadi ya hii ya Christmas kwa kumshukuru Mungu kwa hatua ya mafanikio aliyompa kwa mwaka huu na pili ametoa zawadi hii kwa wadau na mashabiki wake wote wanaondelea kumpa sapoti kwa huduma ya uimbaji anayoifanya hivyo amewataka waendelee kumpa sapoti ya kutosha kwani bado ana vitu vingi vizuri vinavyokuja kwa siku zijazo mwaka 2017.

gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kuupakua wimbo huu wa Merry Christmas(Amezaliwa) kutoka kwa muimbaji Walter Chilambo kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kutangaza Ujumbe huu wa Injili ulio katika wimbo huu na kumpa sapoti mwimbaji huyu na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na Walter Chilambo wasiliana nae kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 718 069 509
Facebook: Walter Chilambo
Instagram: @walterchilambotz

More in Audio

To Top