Connect with us

Walter Chilambo afanikiwa kufunga ndoa, mjini Mbeya

Habari

Walter Chilambo afanikiwa kufunga ndoa, mjini Mbeya

Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Walter Chilambo hatimaye amefanikiwa kufunga pingu za maisha siku ya jana April 14, 2018 na mpenzi wake Loveness Hiza ikiwa ni baada ya kumvalisha pete ya uchumba miezi kadhaa iliyopita.
Walter Chilambo amefikia maamuzi hayo ya kufunga ndoa na mpenzi wake Loveness Hiza baada ya kudumu katika uchumba wao kwa muda mrefu kiasi, hivyo jana April 14 2018 wameripotiwa kuingia rasmi katika ndoa.
Ndoa hiyo imefungwa katika kanisa la Rehoboth international Christian center(RICC) chini ya mchungaji kiongozi Rev.Sunday Matondo lililopo mjini Mbeya.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Walter Chilambo alianza kutambulika kupitia muziki wa Bongofleva, hiyo ni baada ya kipaji chake kuvumbuliwa kwa kuibuka mshindi wa Epic Bongo Star Search 2012(BSS) na kufanikiwa kushinda Tsh milioni 50.
Kwasasa Walter Chilambo anamtumikia Mungu kupitia muziki wa Injili ambapo tayari ameshafanikiwa kuachia nyimbo na video kadhaa ambazo zimempa kibali katika jamii na watu ambao wamekuwa wakiguswa na huduma yake kila iitwapo leo.

Alipangalo Mungu mwanadamu hawezi kulipangua…… Asante @obymack

A post shared by WALTER CHILAMBO (@walterchilambotz) on

Kwa niaba ya uongozi na timu nzima ya gospomedia tunatoa pongezi zetu za dhati kwa muimbaji Walter Chilambo kwa kupiga hatua nyingine nzuri katika maisha yake na mke wake. Waefeso 5:31 –  “Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.”

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top