Habari

Wakristo wanne wa kipastani wameuwawa kwa kupigwa risasi na ISIS, siku ya pasaka

Na Mwandishi wetu,

Kundi la ISIS linadaiwa kuhusika katika shambulio la mauaji na kusababisha vifo vya watu wanne katika familia moja ya Kikristo nchini Pakistani. Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Pasaka katika jimbo la Balochistan nchini Pakistani, karibu na mpaka wa Afghanistani.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja, wote wa familia moja, waliokuwa katika baiskeli ya miguu mitatu (rickshaw) wakisafiri kupitia mji mkuu wa Quetta jimbo la Balochistan walivamiwa na watu wenye silaha za moto na kuwashambulia.

“Watu wanne wameuawa, wote walikuwa wakristo, walipigwa risasi na wamekufa ” Ali Mardan, afisa mkuu wa polisi, aliiambia Al Jazeera.

Waathirika wa tukio hilo, ambao walikuwa wamewatembelea ndugu zao siku ya Pasaka, walikuwa katika kitongoji cha jamii ya wakristo katika mji mkuu wakati wa shambulio hilo.

“Kaka na dada zetu walikuwa wamewatembelea ndugu zao siku ya Pasaka, saa moja baadaye, waliuawa na washambuliaji, msichana mwenye umri wa miaka 12 pia alijeruhiwa katika shambulio hilo.” alisema Khalil Jorge Bhutto, mwanasheria wa Pakistani. ”

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa watu wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara kwa sababu ya imani yao ya kikristo,” Moazzam Jah Ansari, mkuu wa polisi wa jimbo, aliiambia AFP.

“Mambo haya yametosha, sasa ni wakati tunaopaswa wote kusimama dhidi ya magaidi na wauaji hawa.” –  alisema Bhutto.

Takribani asilimia 2 ya idadi ya watu nchini Pakistani ni wakristo, na mara nyingi ndio walengwa wa mashambulizi mengi ya Kiislam.

Mateso mengi ya Wakristo nchini Pakistani hutokea kwenye makundi makubwa ya Kiislam ambayo yamekua na kupanuka huku yakiungwa mkono na kupewa nguvu kupitia vyama vya siasa, jeshi, na serikali,” ilisema Open Doors, ambayo imeitaja Pakistani kuwa kati ya nchi kumi za hatari zaidi duniani kuwa Mkristo.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Elvis Kiwanga - Kweli

Next post

Beatrice Daniel Kuachia Nataka Nitoke Albamu ya DVD