Habari

Wakristo wa kivietinamu washambuliwa, wakilazimishwa kukataa ukristo

Na Mwandishi wetu,

Wakristo ishirini na nne huko nchini Vietnam hivi karibuni walishambuliwa na kikundi cha watu kupinga imani yao.
Tukio lililotokea katika milima ya kaskazini ya nchi hiyo wakati wanakijiji wa kabila linalojulikana kama Hmong walipoamua kumkubali Yesu Kristo, Uongofu wao ulimchochea mkuu wa kijiji ambaye aliwatishia kuwafukuza waumini hao kutoka katika jamii hiyo ikiwa hawakukataa imani yao mpya ya Ukristo, lakini waumini wa Hmong walikataa kufanya hivyo, na ndipo walipovamiwa na kundi la watu na kuwashambulia. 

Kwa mujibu wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Vietnam (VCHR) imesema kuwa mpaka sasa kuna wakristo wanne wapo hospitalini wakiwa na majeraha makubwa ya kichwa na mikono.

Mashambulizi hayo yametokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya mapema mwaka huu ikiipa serikali ya Vietnam nguvu na mamlaka ya kudhibiti shughuli zote za kidini nchini humo.

“Mashambulizi hayo na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya jamii za kikristo vimeongezeka hivi karibuni nchini Vietnam,” VCHR imesema katika taarifa hiyo. “Mamlaka zinakiuka sheria kwa kuzigandamiza shughuli za kidini zilizo rasmi, na kujenga hali ya kutokujali kwa ukiukaji na ukandamizwaji wa uhuru wa dini( imani).”

Licha ya kufunguliwa kwa uhuru wa kisiasa na uchumi nchini Vietnam katika miaka ya hivi karibuni, Bado serikali ya kijamaa(kikomunisti) inahofu juu ya imani za watu nchini humo, lakini hasa dini ya Ukristo, ambayo mara nyingi hutazamwa kwa jicho la mashaka zaidi.

“Sheria imesababisha kuwaathiri wakristo wachache, na utekelezaji wa sheria hiyo katika ngazi ya chini husababisha mateso kutoka kwa viongozi wa mitaa,” ilisema Open Doors, kikundi kinachoangazia uhuru wa kidini duniani kote.

Roman Katoliki ni moja kati ya jamii kubwa zaidi ya kikristo. Hata hivyo, kuna baadhi ya ukuaji wa haraka zaidi wa makanisa hutokea kwa makabila ya mbali kama Hmong. Mara nyingi, makundi haya ya kikabila “hupata mateso makubwa zaidi, hasa katika maeneo ya vijijini” mwa nchi.

“Waumini hawa wanakabiliwa na kutengwa, unyanyasaji, ubaguzi, kupoteza mali na hata mashambulizi ya vurugu kwa imani yao,” ilisema Open Doors, ambayo iliiweka Vietnam katika orodha ya nchi 50 duniani zenye mateso makali zaidi kwa wakristo.

Karibu watu 400,000 kati ya watu milioni moja wa kijiji cha Hmong nchini Vietnam ni wakristo. Kamati ya Haki za Binadamu nchini Vietnam imesema vikwazo vipya kwenye shughuli za kanisa vimelazimisha watu wengi wa Hmong ambao ni wakristo kufanya maamuzi magumu juu ya wapi wanaweza kukusanyika kwa ajili ya ibada.

“Makundi haya madogo ya Kikristo yaliyopo katika maeneo ya milima ya mbali yanalazimishwa kujiunga na madhehebu makubwa, yaliyosajiliwa na serikali,” alisema Vo Van Ai, raisi wa VCHR katika taarifa.

Kwa mujibu wa ripoti zilizochapishwa hivi karibuni zinasema kuwa watu milioni nane kati ya watu milioni 92 walioko nchini Vietnam wanatambuliwa kama wakristo.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mwanafizikia Stephene Hawking kuhifadhiwa katika eneo la kanisa

Next post

Audio: Jay Alain Feat. Okito - Nipe Nguvu