Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Audio: Waba Shadra – Simama Imara

Audio

Audio: Waba Shadra – Simama Imara

Kutoka nchini Norway leo kwa mara nyingine tena nimekusogezea wimbo mzuri uitwao Simama Imara kutoka kwa mwimbaji Waba Shadra, Muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Waba Media Pro.

Simama Imara ni wimbo wa tatu kuachia kwa mwaka 2018, na ni wimbo wa mwisho kutoka kwenye albamu yake iitwayo Mji wa Amani. Wimbo huu unamgusa na kumtia moyo mtu ambaye ameingia kwenye majaribu na mapito ya aina mbalimbali, kupitia wimbo huu mwimbaji Waba Shadra anatukumbusha kusimama Imara katika Imani yetu kwa Mungu ili aweze kutawala na kuongoza maisha yetu hata pale tunapojaribiwa basi asimame kututetea kwa maana yeye ndiyo nguzo yetu.

Mbali ya kuwa mwimbaji na mtayaarishaji wa muziki Waba Shadra pia ni muongozaji(video director) wa video za muziki wa Injili nchini Norway.

Nina imani kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kila utakapokuwa unasikiliza wimbo huu na Bwana Yesu akawe nguzo katika maisha yako, kuanzia sasa, Barikiwa!.

 

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/04/Wabashadra-Simama-Imara.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Waba Shadra kupitia:
Simu/WhatsApp: +47 462 69 248
Facebook: Waba Shadra
Instagram: @wabashadra
Youtube: Waba Media Pro

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 10 ON GOSPOMEDIA

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,309 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top