Audio: Waba Shadra - Neno Moja - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Audio: Waba Shadra – Neno Moja

Audio

Audio: Waba Shadra – Neno Moja

Kutoka nchini Norway mwimbaji Waba Shadra anakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo wake mpya uitwao Neno Moja, muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Waba Media Pro chini ya mikono yake mwenyewe akiwa ndiye prodyuza wa studio hiyo.

Neno Moja ni wimbo wenye kusudi la kuinua mioyo iliyovunjika na kukata tamaa na kusisitiza kuwa watu wasikate tamaa kwakua Neno la Mungu linaweza kwa yeyote anayeamini kupitia jina la Yesu Kristo. Kwa wewe unayetafuta kazi bila mafanikio usikate tamaa, wewe unayesumbuliwa na maradhi ya kila aina usikate tamaa, wewe unayetafuta mtoto bila mafanikio usikate tamaa amini katika Neno la Mungu nalo litatenda muujiza katika maisha yako.

Mbali ya kuwa mwimbaji na mtayaarishaji wa muziki Waba Shadra pia ni muongozaji(video director) mzuri wa video za muziki wa Injili nchini Norway.

Nina imani kuwa utabarikiwa na kuinuliwa zaidi kupitia wimbo huu kila wakati utakapokuwa unasikiliza. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Waba Shadra kupitia:
Simu/WhatsApp: +47 462 69 248
Facebook: Waba Media Pro
Instagram: @wabamediapro
Youtube: Waba Media Pro

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top