Audio

Audio: Waba Shadra – Jina Lako

Kutoka Norway mpaka Tanzania kwa mara nyingine tena mwimbaji Waba Shadra anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya uitwao Jina lako, muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Waba Media Pro chini ya mikono yake mwenyewe.

Jina Lako ni moja ya wimbo unaopatikana kwenye albamu yake mpya inayobebwa na jina la Mji wa Amani ambapo nyimbo hizo kwasasa zinapatikana kwenye channel yake ya YouTube.

Wimbo huu unaelezea jinsi jina la Yesu lilivyo na nguvu ya kubadilisha maisha yetu, tangu miaka mingi iliyopita, leo, kesho na hata milele jina lake bado litaendelea kuwa na nguvu katika kuinua mioyo iliyovunjika na kukata tamaa.

Mbali ya kuwa mwimbaji na mtayaarishaji wa muziki Waba Shadra pia ni muongozaji(video director) wa video za muziki wa Injili nchini Norway kupitia lebo yake Waba Media Pro.

Nina imani kuwa utabarikiwa na kuinuliwa zaidi kupitia wimbo huu, Karibu kupakua. Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Waba Shadra kupitia:
Simu/WhatsApp: +47 462 69 248
Facebook: Waba Media Pro
Instagram: @wabamediapro
Youtube: Waba Media Pro

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Beatrice Mwaipaja - Dhahabu

Next post

Video | Audio: Christina Shusho & Saint Stevoh - Mifupa Mikavu