Connect with us

Vyakula 7 Vinavyoongeza Uwezekano wa Kupata Watoto Mapacha

Vyakula 7 Vinavyoongeza Uwezekano wa Kupata Watoto Mapacha

Dondoo

Vyakula 7 Vinavyoongeza Uwezekano wa Kupata Watoto Mapacha

Kama mara nyingi umekuwa na ndoto ya kutaka kupata mapacha basi weka mazoe ya kula vyakula vifuatavyo na ndoto yako inaweza kutimia. Hivi ni vyakula vinavyoweza kukuongezea nafasi yakushika ujauzito wa watoto mapacha:

Vyakula 7 vinavyoongeza uwezekano wa kupata watoto mapacha

1. Viazi vikuu

Kwenye utafiti mmoja katika kabila liitwalo Yoruba la huko nchini Nigeria iligundulika kwamba katika kabila hilo kuna familia nyingi zenye watoto mapacha.

Na katika kuangalia chakula waligundua kwa sehemu kubwa kabila hili chakula chao kikuu ni viazi vikuu (yams).

Viazi vikuu ni chanzo kikuu cha homoni mbili zinazoweza kuhamasisha kutungwa kwa mimba mapacha zinazojulikana kama ‘progesterone’ na ‘phytoestrogens’.

Kwahiyo, kama upo bize kutaka kupata mapacha tafuta hivi viazi na ufanye kuwa sehemu ya mlo wako mara kwa mara miezi sita hivi kabla ya kuamua kushika ujauzito.

2. Vyakula vyenye folic acid kwa wingi

Folic acid ni moja kati ya madini mhimu sana linapokuja suala la kushika ujauzito na afya nzuri ya ujauzito.

Parachichi na spinachi ni vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira yetu kirahisi na ni vyakula ambavyo ni vyanzo vizuri vya madini haya yanayoweza kupelekea mama kubeba ujauzito wa watoto mapacha.

Wanawake wanaohangaika kupata ujauzito wanashauriwa kupendelea sana kula vyakula hivi.

3. Maziwa au bidhaa zitokanazo na maziwa

Tafiti baada ya tafiti zimethibitisha wanawake na wanaume wanaotumia kwa wingi maziwa, mtindi na bidhaa zingine zitokanazo na maziwa wanakuwa na uwezekano mkubwa mara tano zaidi wa kupata ujauzito wa watoto mapacha.

Kumbuka kama una vidonda vya tumbo usinywe maziwa fresh lakini mtindi unaweza kunywa mara moja moja.

Matumizi ya mara kwa mara ya maziwa au bidhaa zitokanazo na maziwa yanaongeza uwepo wa aina fulani ya protini maalumu ambayo huhusika na kutungwa kwa mimba ya mapacha (‘insulin-like growth factor protein’).

Aina hiyo ya protini inapatikana kwenye maziwa ya ng’ombe na inaweza kupatikana pia kwenye bidhaa zingine za wanyama.

Unapokunywa maziwa fresh mara kwa mara mirija yako ya mayai inao uwezo zaidi wa kutoa yai zaidi ya moja ili kurutubishwa na hatimaye kukupa watoto mapacha.

4. Mizizi ya Maca

Maca ni aina nyingine ya vyakula mhimu sana kwa wanawake na wanaume wanaotafuta ujauzito.

Maca inapendekezwa kwa wanawake wanaotamani kupata ujauzito wa watoto mapacha kwani inahusika sana na kuimarisha afya ya uzazi kwa ujumla kwa mwanamke.

Ingawa hakuna ushuhuda wa wazi juu ya maca na mapacha bado kujaribu hakutakuharibu chochote.

Mizizi ya maca unaweza kuipata ikiwa mizizi au ikiwa katika unga au hata katika vidonge maalumu.

5. Wanga unaomeng’enywa pole pole (Complex Carbohydrates)

Aina ya vyakula vya wanga unavyokula vinao uwezo wa kukuongezea nafasi ya kupata mimba ya watoto mapacha.

Vyakula vya wanga unaomeng’enywa pole pole ni pamoja na maharage, nafaka zisizokobolewa na mboga za majani.

Mwili wako humeng’enya vyakula kama biskuti, keki, mkate mweupe na wali mweupe kwa haraka sana na kuvibadili kuwa glukozi (damu sukari).

Ili kuiondoa hii damu sukari kwenye damu kongosho huongeza insulin kwenye damu na tafiti zinaonyesha kiasi kingi cha insulin kwenye damu yako kinasababisha kutungwa ujauzito kuwa kibarua kizito.

Wanga mzuri ni ule wenye nyuzinyuzi nyingi (fiber) kama vile mkate ambao unga wake haujakobolewa (brown bread), ugali wa dona, maharage, matunda na mboga za majani.

Vyakula vya wanga vya namna hii vina matokeo mazuri kwa damu sukari (kisukari) na insulin.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top