Video | Audio: Wagala Music - Wewe ni zaidi - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Wagala Music – Wewe ni zaidi

Audio

Video | Audio: Wagala Music – Wewe ni zaidi

Mwimbaji anayeendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili kutoka jijini Dar es salaam Wagala Music ameachia video yake mpya ya wimbo uitwao “Wewe ni zaidi” ikiwa imeongozwa na director Jukya na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Chief Elia na kurekodiwa ndani ya studio za Success Music.

Wewe ni zaidi ni wimbo uliobeba maombi ya kumtafakari na kumshukuru Mungu kwa uwezo wake mkuu na kwa yale ambayo ameyatenda katika maisha yetu.

“Yesu ni zaidi ya kila kitu katika maisha yetu, yeye ni zaidi kwakuwa alikubali kuteswa na kufa msalabani ili mimi na wewe tukombolewe kutoka kwenye utumwa wa dhambi, Yeye ni zaidi kwakuwa amekuwa akisimama na sisi katika kila hatua ndani ya maisha yetu, Yeye ni zaidi kwakuwa upendo wake ni mkuu na wenye kutenda maajabu sana kiasi ambacho hatuwezi kulipa gharama yake, Yeye ni zaidi ya vyote.” – alisema Wagala

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Wagala Music kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 340 699
Facebook: Wagala Hamidu
Instagram: @wagala_music
Youtube: wagala Music

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top