Video
Video | Audio: Mwamini Muyero – Yesu Usifiwe
Baada ya siku chache zilizopita kuachia wimbo wake mpya uitwao Yesu Usifiwe mwimbaji wa nyimbo za Injili Mwamini Muyero leo ameachia video ya wimbo huo ikiwa imeongozwa na director Mbangwa Hassan, ukiwa ni wimbo maalum wa sifa kwa ajili ya Pasaka, Muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za Soft Records chini ya mikono ya prodyuza Pitshou Mesha.
“Yesu Usifiwe ni wimbo wa Sifa nikiwakumbusha watu, hasa wale wanaopitia katika shida na mambo magumu, wimbo huu ukawe nuru na nguzo ya matumaini katika maisha yao na nawasihi watambue kuwa hakuna lisilowezekana kwa Yesu maana yote aliyamaliza pale msalabani, waendelee kumtumainia Mungu naye atatenda miujiza kwa zaidi ya wanavyofikiria, Ameen.” – Mwamini Muyero
Ikumbukwe kuwa mwimbaji Mwamini Muyero tayari ana albamu iitwayo Nimepata Pumziko aliyoachia mwaka 2016 ikiwa kwenye mfumo wa Audio CD na DvD ikiwa inasambazwa na yeye mwenyewe na kupatikana kwenye maduka ya wasambazaji kote nchini.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu hapa nikiamini kuwa utabarikiwa zaidi, Ameen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Mwamini Muyero kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 769 698 909
Facebook: Mwamini Muyero
Instagram: @officialmwamini
YouTube: Mwamini Muyero
Like us on facebook >> GOSPO MEDIA Follow us on instagram >> @gospomedia
