Connect with us

Video kumi bora zilizofanya vizuri mwezi oktoba 2017, hizi hapa.

Muziki

Video kumi bora zilizofanya vizuri mwezi oktoba 2017, hizi hapa.

Katika mwezi wa kumi tumeshuhudia video mbalimbali za waimbaji wa nyimbo za Injili zikiachiwa kutoka ndani na nje ya Tanzania na hakika nyingi kati ya video hizo zimekuwa na mguso wa kipekee na viwango vya kuridhisha ikiwemo Subiri(Wait) iliyomhusisha Mercy Masika, Emmy Kosgei na Evelyn Wanjiru ikiwa ni moja ya video iliyotikisa kiwanda cha muziki wa Injili afrika mashariki kwa mwezi wa kumi pamoja na video nyingine nyingi ikiwemo ile ya Nipokee kutoka kwa J Sisters, Lihimidi Jina lake kutoka kwa Joyce Omondi na nyinginezo ambazo pia zimefanikiwa kuingia kwenye chati hii kupitia tovuti yako pendwa gospomedia.com.

Na hizi hapa ni orodha kamili ya video 10 bora za muziki wa Injili zilizofanya vizuri zaidi mwezi wa oktoba 2017.

1. Mercy Masika, Emmy Kosgei & Evelyn Wanjiru – Subiri(Wait)

2. J Sisters – Nipokee

3. Joyce Omondi – Lihimidi jina lake

4. Rogate Kalengo – Kuna Namna

5. Eddah Mwampagama Feat Walter Chilambo – Unajuaga

6. Bomby Johnson – Hakuna Jambo

7. Ritha Komba – Nitashinda

8. Alphee Niyo – Songa Mbele

9. Sakina Naftali – Yatakwisha

10. Bertha Kapufi – Maombi

Uongozi na timu nzima ya idara ya muziki ya gospomedia.com inatoa pongezi kwa wanamuziki na waimbaji wote ambao video zao zimeonekana kufanya vizuri zaidi mwezi oktoba na kuwabariki watu wengi zaidi, Mungu awabariki sana.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top