Video

Video | Audio: Goodluck Gozbert – Hauwezi Kushindana

Kutoka kwenye albamu yake mpya iitwayo ”Shukurani” moja kati ya mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla Goodluck Gozbert ambaye siku chache zilizopita aliachia wimbo kutoka kwenye albamu hiyo leo ameachia video ya wimbo huo uitwao Hauwezi kushindana ukiwa ni wimbo wa tatu kutoka kwenye albamu hiyo ambayo ina mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa katika mfumo wa Audio CD.

Video hii imeongozwa na director Director Destro na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Paulo kutoka jijini Nairobi Kenya.

Goodluck Gozbert ni moja kati ya waimbaji wa kizazi kipya cha muziki wa Injili nchini Tanzania aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana kazi zake nzuri za muziki zinazoendelea kudhihirisha uwezo wake kiuimbaji na tungo  zenye kumsifu Mungu na kuinua nafsi na mioyo ya watu wengi mpaka kufanikiwa kunyakua tuzo kadhaa ambazo kwa hakika zimempa mafanikio makubwa kimuziki.

Albamu ya Shukurani kwasasa inapatikana sokoni waweza kupata nakala yako kupitia wakala wa Max Malipo waliopo sehemu mbalimbali nchini Tanzania.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na muimbaji Goodluck Gozbert kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 655 212 720 au +255 654 276 560​⁠​
Facebook: Goodluck Gozbert
Instagram: @goodluckgozbert
Youtube: Goodluck Gozbert
Twitter: @goodluckgozbert
Website: www.goodluckgozbertministry.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Sampamba - Roho Mtakatifu

Next post

Audio: AD Music Feat. Happy - Imara