Connect with us

Video | Audio: Benedict Fanuel – Baraka

Video

Video | Audio: Benedict Fanuel – Baraka

“Baraka kila mtu ameandikiwa na Mungu na hakuna mtu asiyependa kubarikiwa, wimbo huu unazungumzia baadhi ya baraka ambazo ni wajibu wetu kuzipata kama tulivyoambiwa kuwa tutabarikiwa shambani pamoja na mijini, tuingiapo na tutokapo Baraka zitaambatana pamaja nasi. Naamini ukichukua muda wako mfupi kusikiliza wimbo huu utagundua ni Baraka gani hasa zinazozungumziwa, watu hawapendi kukuona ukibarikiwa, ukifanikiwa na wengine kukusemea maneno mabaya ilimradi baraka zako zisikufikie ila neno la Mungu halijawahi kubadilika kama Baraka yako ipo basi ipo tu, Mungu akubariki sana!. ” – Alisema Benedict Fanuel.

Hii ni video ya wimbo uitwao Baraka kutoka kwa mwimbaji Benedict Fanuel, video hii imeongozwa na director Ajez na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Makarithym kutoka ndani ya studio za Trust Music Lab.

Benedict Fanuel ni moja kati ya waimbaji wapya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akitokea jijini Dar es salaam ambaye ameanza kuonekana kufanya vizuri toka mwaka 2017 akiwa chini ya menejimenti ya Trust Music Lab, na hii ikiwa ni kazi yake mpya kwa mwaka 2018 tunayoaamini itakwenda kumvusha hatua moja kwenda nyingine.

Mungu akupe Baraka kila utakapokuwa unausikiliza wimbo huu utakaokufanya umtafakari Mungu kwa kiwango cha utukufu wa juu kabisa. Karibu ubarikiwe!.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Benedict Fanuel kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 713 606 038, +255 655 334 949
Facebook: Benedict Fanuel
Instagram: @benanto_tz
Youtube: Benedict Fanuel

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

To Top