Connect with us

Video | Audio: Ben william – Nakupenda

Audio

Video | Audio: Ben william – Nakupenda

Kutoka jijini Mwanza leo tumekusogezea video ya wimbo uitwao Nakupenda kutoka kwa mtumishi wa Mungu, mwimbaji na mtayaarishaji wa nyimbo za Injili maarufu kama Benny William. Video hii imeongozwa na director Einxer na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Apex Music.

Nakupenda ni wimbo uliojaa sifa kwa Mungu ukitukumbusha na kusisitiza juu ya Upendo wetu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametupenda hata akajitoa ili ateswe na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na hata baada ya kufufuka kwake bado upendo wake unaendelea kutawala maisha yetu hadi sasa.

Kila mmoja sasa kwa nafasi yake apate muda wa kutafakari upendo wa Mungu na kujitathmini ndani ya nafsi yake juu ya upendo wake kwa Mungu kupitia matendo yake.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii njema tukiamini kuwa utaguswa na kubarikiwa zaidi!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ben William kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 719 813 124
Facebook: Benny William
Instagram: @bennywilliam_Official
Youtube: Ben William

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top