Connect with us

Video | Audio: Asacs Choir – Getseman

Video

Video | Audio: Asacs Choir – Getseman

Leo ikiwa ni siku ya Ijumaa kuu tukitafakari mateso ya Yesu, kutoka mkoani Sumbawanga nimekusogezea video ya wimbo uitwao Getseman ulioimbwa na kwaya iitwayo Asacs Choir, video hii imeongozwa na kampuni ya Asacs video production.

Getseman ni wimbo maalumu kwa ajili ya kutafakari mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na wakati huu ni wakati wa jitafakari na kujitathmini juu ya matendo kwa Bwana, na pale ambapo tumetenda dhambi basi yatupasa kufanya toba ili tupate kutakaswa upya na kujenga kanisa jipya ndani ya mwili wa kristo.

Ni hakika utabarikiwa kwa kuitazama video hii ambayo wimbo wake umejaa mafuta ya kukufanya utafakari mateso na kufa kwa Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani ikidhihirisha alama ya upendo wake mkuu kwetu sisi wanadamu, ambapo kwa damu yake sisi tumekombolewa, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na uongozi wa Asacs Choir kupitia:
Simu/WhatsApp:
Facebook:
Instagram:

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

To Top