Video

Music Video | Audio: Vaileth Mwaisumo – Umebaki Mwenyewe

Kutoka mjini Iringa leo kwa mara ya kwanza naitambulisha kwako video iitwayo Umebaki Mwenyewe kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Vaileth Mwaisumo. Video ya wimbo huu imeongozwa na director mahiri anayefahamika kwa jina la Debro Gabriel na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Eck Production chini ya mikono ya prodyuza Eck Nyongoto kutoka jijini Dar es salaam.

Umebaki Mwenyewe ni wimbo uliobeba ujumbe mkubwa wa matumaini kwa watu wote ambao wanapitia magumu kwa muda mrefu bila majibu. Kupitia sauti na kipawa alichokiweka Mungu kwa mtumishi wake Vaileth Mwaisumo na kumbariki kuja na wimbo huu ili akutie moyo wewe ambaye unahisi kuchoka na kukata tamaa kutokana na magumu unayopitia kiuchumi, familia, mahusiano, kazi, biashara, magonjwa yasiyokwisha na mambo mengi yanayokuzonga leo kupitia wimbo huu kiri ushindi na kwa kinywa chako tamka baraka ya kufunguliwa kutoka kwenye vifungo vinavyokurudisha nyuma maana hakuna aliyebaki kukusaidia zaidi ya Yesu Mwenyewe.

Akizungumza na gospomedia.com kuhusu wimbo huu mtumishi Vaileth alikuwa na haya ya kusema:

”Lengo la wimbo huu ni kumkimbilia MUNGU wakati wa shida na kujua kwake pekee ndio kuna msaada wa kweli, Wanadamu wanaweza kukuacha lakini sio MUNGU kamwe hawezi kukuacha. Geuza macho yako muangalie YESU wakati wa tabu na majaribu.” – Alisema Vaileth Mwaisumo.

Ni imani yangu kwamba utabarikiwa na video hii iliyosheheni uhalisia wa kile kinachozungumzwa na kukusudiwa na hakika utabarikiwa na kuinuliwa na wimbo huu kila utakapokuwa unausikiliza, Kupitia roho mtakatifu Yesu Kristo akusaidie pale ambapo unahisi ugumu wa jambo lako. Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Vaileth Mwaisumo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 838 052
Facebook: Vaileth Mwaisumo
Instagram: @vailethmwaisumo Youtube: Vaileth Mwaisumo

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Audio: Evacia Cathles - Mataifa Yote

Next post

Music Audio: God Surrender's - Walioitwa | Imeandikwa