Habari za Muziki

Usiku wa HipHop Takatifu kufanyika 18 Mei 2018

Kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop lijulikanalo kama Yesu Okoa Mitaa(Y.O.M) wanatarajia kufanya tamasha kubwa la muziki wa Injili liitwalo Usiku wa HipHop Takatifu(The Night of Holy HipHop) litakalofanyika tarehe 18.05.2018 katika ukumbi wa kanisa City Worship Centre(CWC) lililopo Tabata Kimanga majichumvi kuanzia saa tatu usiku mpaka asubuhi.

Tamasha hilo litasindikizwa na rapa zaidi ya 20 kutoka katika kundi hilo ambao wote watahudumu katika madhabahu itakayosimamiwa na jopo la wachungaji, mitume na manabii litakaloongozwa na senior Pastor Timothy Mwita huku mgeni rasmi akiwa ni Mheshimiwa David Robert Mwamsojo.

Akiongea na gospomedia.com Kiongozi wa kundi la Yesu Okoa Mitaa Rungu la Yesu amesema kuwa mwaka huu wamejipanga vizuri kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa na kwa uwezo wa Mungu anaamini Mungu atatenda mambo ya kihistoria kwa ajili ya watu wa Mungu siku hiyo.

Mbali na kuzungumzia nguvu ya tamasha hilo, Amewasisitiza watu wote kutoka kila pembe ya jiji la Dar es salaam na mikoa ya jirani kufika siku hiyo ili kupokea baraka za Mungu zitakazoacha historia katika maisha yao.

Kwa mawasiliano zaidi na jinsi ya kufika wasiliana na uongozi wa kundi la Yesu Okoa Mitaa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 348 032
Facebook: Yesu Okoa Mitaa
Instagram: @yesuokoamitaa
Youtube: Yesu Okoa Mitaa

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Benachi - Nikumbuke

Next post

Video | Audio: Elandre - Mwamba