Usiku wa Hip Hop Takatifu na Yesu Okoa Mitaa Wafana - Gospo Media
Connect with us

Usiku wa Hip Hop Takatifu na Yesu Okoa Mitaa Wafana

Habari

Usiku wa Hip Hop Takatifu na Yesu Okoa Mitaa Wafana

Na Mwandishi wetu,

Usiku wa Hip Hop Takatifu ulioandaliwa na huduma ya Yesu Okoa Mitaa (YOM) tarehe 18 Mei, wafana. Usiku huo uliokuwa na lengo la kutangaza Injili kwa njia ya muziki wa aina ya hip hop uliohudhuriwa na wageni kadhaa kutoka madhehebu tofauti jijini Dar es Salaam .

Historia inaonyesha  muziki wa hip hop ulichukua kasi kuanzia miaka ya 1980 hata hivyo haukupokelewa vizuri sana makanisani nchini Tanzania kama njia ya kuhubiri injili kwa vijana kama ilivyo hivi sasa .

Mh. David Robert, Mgeni rasmi akizungumza jambo katika tukio hilo la Usiku wa HipHop Takatifu.

“Kuna wachungaji walitupinga sana na kutuona tunapotosha vijana ” alinukuliwa Mh. David Robert Mwamsojo nguli wa muziki wa injili Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi katika usiku huo .

David  alitamba sana miaka ya 2000 kupitia nyimbo zake. Wimbo wa Bwana atafanya njia na Kiganjani pa Mungu uligusa wengi na kubadilisha maisha ya vijana akiwemo Rapper Peter Banzi ambaye usiku huo alikabidhiwa tuzo ya heshima pamoja na waimbaji wengine wa Gospel hip hop kufuatia mchango wao katika kuuendeleza harakati hizo kupitia injili.

Baadhi ya waimbaji, watangazaji na wadau wengine waliopewa tuzo usiku huo alikua mwimbaji Emmanuel Mbasha , David Robert ,Meshack , Baltazary Morefire, Kuhani Zangina , Gospo Media , Hossein Gabriel na Dj Supremacy kutoka Praise Power Radio.

Rais wa huduma ya Yesu Okoa Mitaa Rungu la Yesu akisema neno.

Kwa mujibu wa Rais wa YOM ministry rapper Rungu la Yesu alimwelezea mgeni rasmi kupitia risala yake jinsi muziki wa gospel hip hop unavyogusa maisha ya wengi kwa sasa hususani vijana na wengi kuweza kuamini injili pamoja na kubadilishwa maisha yao akiwemo rapper maarufu wa kundi la hard blasters – Fanani ambaye ameamua kumfuata Yesu hivi karibuni .

Katika picha ya pamoja Rais wa Yesu Okoa Mitaa Rungu la Yesu(kushoto) akiwa na mgeni rasmi katika tukio la Usiku wa HipHop Mh. David Robert.

Mbali na hayo Mgeni rasmi David Robert ameipongeza huduma ya Yesu Okoa Mitaa kwa dhamira yao ya ndani katika kuokoa kizazi cha vijana wa kipindi hiki kutoka katika mikono ya shetani kwa kubuni njia ya kufanya muziki wa Hip Hop kumwimbia Mungu ili vijana waokoke na ameahidi kuwaunga mkono kwa kuwapatia shilingi milioni moja kila mwaka ili waweze kuiboresha huduma hiyo ili iweze kuwafikia vijana wengi zaidi ndani na nje ya Tanzania

Picha na taarifa hii imeletwa kwenu kwa hisani ya Erasmus Kamugisha kutoka EK Studios, Christ Worship Center, Gospo Media, na Praise Power Radio.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top