Uncategorized

Usikose Kongamano Kubwa la Vijana na Wanafunzi “Ambassadors Mega Fest” Tarehe 08 Nov – 11 Nov 2016.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God(T.A.G) wanakuletea kongamano kubwa la Vijana na Wanafunzi linaloitwa Ambassadors MEGA FEST litakalofanyika kuanzia tarehe 8.11.2016 mpaka tarehe 10.11.2016 katika ukumbi wa CHIMWAGA HALL UDOM Dodoma, ambapo vijana na wanafunzi watajiandikisha kuingia kambini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu vijana na wanafunzi ikiwa ni pamoja na neno la Mungu, ada ya kujiandikisha kwa ajili ya kuingia kambini hapo ni shilingi 30,000/- kwa mtu wa kawaida na shilingi 25,000/- kwa wanafunzi.

Wanenaji na wahubiri katika kongamano hilo ni pamoja na Mchungaji Sylvester Putaputa, Mchungaji Godwin Mjack na Mchungaji Dr.Huruma Nkone kutoka kanisa la VCCT Dar e salaam na itakapofika ijumaa ya terehe 11.11.2016 kutakuwa na tamasha kubwa la vijana na wanafunzi (Ambassadors Mega Night) katika viwanja vya jamhuri dodoma kuanzia saa moja usiku mpaka asubuhi.

Waimbaji  watakaohudumu siku ya tamasha hilo ni pamoja na Dodoma Student Mass Choir, Rivers of Joy International(VCC Dar es salaam) na waimbaji wengine wengi, watakaohubiri siku ya tamasha hilo ni pamoja na Mwinjilisti wa kimataifa kutoka sweden Eve.Johannes Amrizer pamoja na Askofu mkuu Bish.Barnabas Mtokambali kumbuka hakuna kiingilio siku ya tamasha hili kubwa la wanafunzi na vijana Ambassadors Mega Night. Wote Mnakaribishwa sana!!

SIKILIZA ZAIDI HAPA

Kwa mawasiliano zaidi juu ya Kongamano na Tamasha hili na jinsi ya kufika piga simu au whatsapp kupitia:
+255 755 336 906 au +255 715 572 461

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mpigie kura Mwimbaji Beatrice Kitauli kwenye Tuzo za Xtreem. Maelekezo yako hapa..

Next post

Download Music Audio: Beatrice Kitauli feat Rose Muhando-Kesho