Habari

Usanifu Experts Videoz Watoa Ofa ya Video Production Kwa Waimbaji Wa Muziki Wa Injili.

Kampuni ya uzalishaji wa video za muziki wa Injili nchini Tanzania Usanifu Experts Videoz, wametangaza rasmi ofa maalumu ya punguzo la gharama ya huduma hiyo kwa waimbaji wote wa muziki wa Injili Tanzania ambapo muimbaji atakayehitaji ofa hiyo atalipa kiasi cha shilingi milioni moja tu na kufanyiwa rekodi ya nyimbo nane badala ya milioni mbili kama ilivyokuwa kwa gharama za awali.

Akiongea na gospomedia.com director wa kampuni hiyo ya uzalishaji wa video Bw. Davishija amesema kuwa ameamua kutoa ofa hiyo kwa waimbaji wote ambao wana bajeti ndogo za uandaaji wa video zao hivyo amejiandaa  vyema kuhakikisha anapokea kazi za waimbaji hao na kuhakikisha zinakuwa kwenye kiwango kizuri cha ubora kwa gharama ambayo wataweza kuimudu.

Ofa hii itakuwa ni ya msimu wa nane nane hivyo amewasihi waimbaji wote ambao watahitaji ofa hiyo wafanye hima kupata fursa hii ambayo anaamini itawapunguzia mzigo wa gharama ambazo kwa namna moja ama nyingine zinawakwamisha kufikia malengo yao. Alisema director Davishija.

Moja ya video ambazo zilimefanywa na kampuni hiyo ni pamoja na hii hapa chini kutoka kwa muimbaji Florence Mackenzi wimbo unaitwa Ipo Faida.

Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kupata ofa hii wasiliana na Usanii Experts Videoz kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 621 32 00 32 au +255 714 50 03 23

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Deitrick Haddon Aachia Video yake Mpya - Come By Here. Itazame Hapa.

Next post

Download Music Audio: Varkeize Motema Feat Daisy & Larry Singlive - Hear Our Cry