Uncategorized

UFAHAMU UKRISTO NA DINI ZA ULIMWENGU.

Tangu mwanzo wa karne ya 21, Ukristo una wafuasi wanaokadiriwa Bilioni 2.2 kati ya watu Bilioni 7.2 dunia nzima. Imani hii inawakilisha 1/3 (moja ya tatu) ya hesabu ya dunia, na ndiyo dini kubwa duniani ikiwa na makundi makuu matatu ambayo ni Makanisa ya Katoliki, Waprotestanti na Makanisa ya Magharibi ya Orthodox. Dhehebu kubwa kutokana na uchunguzi ni Kanisa Katoliki likiwa na wafuasi Bilioni 1.09 na kundi la pili ni ama Protestanti (wanahesabiwa kama kundi moja) ama kanisa la Orthodox (Kama waprotestanti wakiwa wamegawanyika katika madhehebu kadhaa, Orthodox watakuwa ni wengi Zaidi)

Ukristo ni dini kubwa pia Ulaya (Europe), Russia, kwa Wamarekani, Kwa Wafilipino, Timori Mashariki, Kusini mwa Afrika, Afrika ya kati, Afrika Mashariki na Oceania. Pia kuna jamii kubwa za Kikristo katika baadhi ya maeneo duniani kama Asia ya Kati na pia mashariki ya Kati ambapo Ukristo ni dini kubwa ya pili baada ya Uislamu. Marekani ndiyo nchi yenye Wakristo wengi duniani ikifuatiwa na Brazili na Mexico.

Katika baadhi ya Nchi Ukristo ni mfumo unaotawala Majimbo katika nchi 15, hizi hapa:-

 1. Argentina (kanisa katoliki).
 2. Tuvalu (kanisa la Tuvalu).
 3. Tonga (free Wesleyan church of Tonga).
 4. Costa Rica (kanisa katoliki).
 5. Ufalme wa Denmark (danish national church).
 6. England (church of England).
 7. Ugiriki (eastern orthodox church).
 8. Georgia (eastern orthodox church).
 9. Iceland (church of iceland).
 10. Liechtenstein (kanisa katoliki).
 11. Malta (kanisa katoliki).
 12. Monaco (kanisa katoliki).
 13. Norway (kanisa la Norway).
 14. Jiji la Vatican (Kanisa Katoliki).
 15. Zambia.

Haya ni makadirio ambayo hayapishani sana na ukweli halisi

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

DOWNLOAD AUDIO: REBECCA MABALA-POKEA SIFA NA UTUKUFU

Next post

SABA WAOKOKA KWENYE USIKU WA GOSPEL HIP HOP, WENGI WAFUNGULIWA KWENYE VIFUNGO.