Habari

Ufahamu Ukimya wa Daudi Mpemba Wangu Wenye Manufaa Makubwa Kwa Mashabiki.

Pamoja na kuwa kimya kwa kipindi kirefu sasa tangu alipoachia wimbo wake Mnyang’anye shetani  mwimbaji Daudi Mpemba amesema ukimya wake unatokana kuuachia wimbo wake huo ili uwafikie watu wengi kwa muda wa kutosha.

Akizungumza na Gospo Media alisema kuwa kwa kipindi hiki ametulia kwanza ili wimbo wake huo upate nafasi na uweze kufika mbali zaidi.

Nachotaka kusema hapa  na nieleweke hivyo kuwa kwa nia nzuri kabisa nimechelea kuachia wimbo mwingine kwasababu tu,wimbo huo wa Mnyang’anye shetani umepokelewa vizuri na wadau wanauelewa vizuri sana sasa nikitoa mwingine hapa naweza wachanganya watu bure kabla huu haujafika mbali kuachia mwingine ni kuwachanganya wadau wa muziki wetu kitu kizuri ni kuwa ukiimba hapa Dar basi hata ukienda Mwanza au Arushaa watu wawe wanaimba na wewe Mnyang’annye shetani na sio Dar wanakujua kwa wimbo mwingine Mbeya nao wanakufahamu kwa wimbo mwingine huko ni kuwachanganya watu na kuwapa wakati mgumu Mashabiki wetu“Alisema Daudi Mpemba.

Mwimbaji huyo mwenye Albamu moja mpaka sasa yenye jumla ya nyimbo Tisa inayofahamika kwa jina la Mnnyang’anye shetani ambayo inaapatikana mikononi mwake mwenyewe.

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko na mwimbaji Daudi Mpemba wasiliana naye kupitia
Simu/WhatsApp: +255 658 148 866
Facebook: Daudi Mpemba
Instagram: @daudimpmba

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Ikupa Mwambenja Auzungumzia Wimbo Wake wa Uzuri Wako, Audio Pamoja na Video Yake.

Next post

Jacob Sanke Kuzindua Albamu Yake Mpya Siku Zinakuja March 26/2016 Dar es Salaam.