Connect with us

Uchaguzi Mkuu CHAMUITA kufanyika Tarehe 29 Septemba 2017.

Habari

Uchaguzi Mkuu CHAMUITA kufanyika Tarehe 29 Septemba 2017.

Raisi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) Bw.Addo November ametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika tarehe 29 Septemba 2017. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bw.Addo Novemba ameandika “Jamani ndugu viongozi na wanachama wa Chama Cha Muziki wa Injili… kutokana na kasi ya Rais wetu Magufuli… nikiwa Rais wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania natangaza Uchaguzi Mkuu wa CHAMUITA Ijumaaa tarehe 29 Mwezi wa 9. 2017, nafasi zinazogombewa ni 1. Rais wa Chamuita  2. Makamu 2. Katibu Mkuu 3. Naibu Katibu Mkuu 4. Katibu Mwenezi 5. Naibu Katibu Mwenezi 6. Mtunza Hazina 7. Mtunza Hazina Msaidizi, 8. Nafasi za Wajumbe 10.
Fomu zitapatikana kuanzia Alhamisi  tarehe 7/9/2017 Fomu ya uraisi ni 70,000/= Makamu ni 60,000/=, Katibu ni 50,000/=, Naibu Katibu Mkuu 40,000/=, Katibu Mwenezi na Makamu wake ni 40,000/=, Mtunza Hazina na Mtunza Hazina Msaidizi ni 40,000/=,

Wajumbe nafasi 10, fomu elfu 20,000/=
Lengo kuu ni kuhakikisha tunakiimarisha Chama Chetu pia kiwe shirikishi na kiongeze wapenzi na wanachama. Mungu awabariki sana Chukueni fomu tukabidhi uongozi kwa amani kwa watakaochaguliwa.
*KUMBUKA CHAMUITA NI YAKO MWANACHAMA.*
Sifa  za kugombea  uongozi uwe mwanachama hai wa Chama Chama Cha Muziki Injili. Binafsi nawashukuru viongozi wote waliokua madarakani yeyote anayependa kuendelea na uongozi agombee binafsi natamani kukabidhi madaraka kwa mtu mtakayemuona anafaa kuwa Rais Mpya wa Chamuita.
Kuhusu Kuchukua Fomu nitawajulisha “stay tuned”(Kaa tayari).
*Wasambazie taarifa hii watu wengi  iwezekanavyo ili ujumbe huu ufike nchi nzima.*
Wasalaam Addo November Mwasongwe 

Raisi CHAMUITA +255 754 396 367” hivi ndivyo alivyomaliza kuandika kupitia ukurasa wake huo.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top