Connect with us

Tumieni Nyumba za Ibada Elimu Chanjo ya Corona

Tumieni Nyumba za Ibada Elimu Chanjo ya Corona

Habari

Tumieni Nyumba za Ibada Elimu Chanjo ya Corona

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri, amewaomba viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kutoa elimu ya chanjo ya UVIKO-19, ili wananchi wengi wachanje, kujikinga na ugonjwa huo.

Sara aliyasema hayo jana, wakati akifungua kikao cha afya ya msingi kilichofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha. Alisema viongozi wa ngazi mbalimbali waliopata elimu ya UVIKO-19 wanatakiwa kuifikisha kwa wananchi na kwa viongozi wa dini wanatakiwa kuwaelimisha waumini wanaofika kwenye ibada. “Viongozi wa dini wamekuwa wakiisaidia serikali katika vitu mbalimbali, ikiwamo kuiombea nchi kwakuwa wananchi wengi wanafika kwenye
nyumba za ibada ni vyema wakaelezwa ukweli kuhusu chanjo hii na mwenye hiari aweze kuchanjwa,” alisema.

Aidha, alisema wilaya hiyo imejipanga kuwafikia wananchi wote watakao kuwa tayari kuchanjwa popote walipo.
Mratibu wa chanjo Wilaya ya Kibaha, Hadija Tellack, alisema wilaya hiyo ilipokea chanjo 7,000 na hadi sasa wataalamu wa afya wanaendelea kuchanja wananchi katika vituo 46 vinavyotoa huduma hiyo.

Kwa upande wa mkoa zilipokelewa chanjo 30,000 na hadi sasa 15,000 zimetumika na inaelezwa kuwa umesalia mwezi mmoja wa matumizi ya chanjo hizo kabla ya kuharibika. Mkuu wa Mkoa wa Pwani alieleza hivi karibuni kuwa wapo wataalamu 554 wamepata mafunzo ya kutoa chanzo na watawafikia wananchi ngazi zote hadi majumbani kwa wenye hiari ya kuchanja watafikiwa.

Chanzo: IPP

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top