gospomedia.com ni tovuti  inayorusha habari za njema za Injili, nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Lengo kuu la kuanzishwa kwa tovuti hii ni kusaidia jamii kupata ufahamu na kushuhudia habari njema za Bwana wetu Yesu Kristo duniani kote, Ikiwa ni mkakati maalumu wa kuihamasisha jamii kuacha maovu na kuwa karibu na Mungu, kudumisha amani na upendo ndani ya jamii na taifa kwa ujumla bila kujali dini, kabila, au jinsia.

Kupitia mafundisho ya kiroho, mahubiri na makala za maarifa ya kijamii kama vile afya, vijana, uchumi, mahusiano, sheria n.k jamii itapata kufunguliwa kiroho na kimwili kwa kupokea maarifa mapya.

Mbali na hayo tovuti hii pia inazisaidia taasisi mbalimbali za kidini kama vile makanisa, mashirika na watumishi wengine binafsi kuitangaza Injili kupitia huduma zao ili jamii ipate kukombolewa.

Advertisements