Audio

Audio Music: Tonia Shodunke – Most high God

Baada ya kuachia wimbo uitwao ”My Rock” mapema mwaka huu aliomshirikisha mwimbaji wa kimataifa Isabella Melodies, na sasa mwimbaji Tonia Shodunke kutoka nchini nigeria amekuja na ujio wake mwingine uitwao Most High God, muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Phat E.

Most High God ni wimbo unaopatikana kwenye albamu yake ya nne inayotarajiwa kuachiwa mapema 2018 ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo zenye sifa na utukufu kwa Mungu kwa kiwango cha kipekee zinazotarajiwa kutengeneza mioyo ya watu kuwa yenye unyenyekevu na hofu kwa Mungu.

“Most High God” ni wimbo wa ushindi, wimbo wa ibada wenye kuvutia ukieleza asili ya kipekee ya Mungu mwenye nguvu na maajabu yake ya kustaajabisha. Nina imani kwamba baada ya kusikiliza wimbo huu utabarikiwa na vita vyako vitageuka kuwa ushindi. Ameen!

 

Download Audio

Social Media
Facebook: Tonia Shodunke
Instagram: @toniashodunke
Twitter: @toniashodunke

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Audio: Abraham K - Stronger

Next post

Music Audio: Neema Ng'asha - Kheri ya Krismasi na Mwaka Mpya