Connect with us

Tofauti sita kati ya funga ya Waislamu na ile ya Wakristo

Kufunga waislam vs Wakristo_BBC

Dondoo

Tofauti sita kati ya funga ya Waislamu na ile ya Wakristo

Kuna tofauti kati ya funga ya Waislamu na ile ya Wakristo licha ya kwamba wote wanatekeleza nguzo hiyo muhimu ili kuwa karibu na Mungu.

Wasomi wengi wamekuwa wakisema kwamba tofauti hizo zinashirikisha hatua ya Waislamu kufunga kwa siku 29 au 30 kulingana na hadithi za mtume Muhammad kwamba mwezi katika Uislamu huchukua siku 30 au 29 hivyobasi kufunga kunaweza kushirikisha siku 29 au 30.

Lakini ushahidi pia unaonesha kwamba katika Ukristo wao hufunga kwa siku 40 kwasababu wanaamini kwamba Yesu alikaa siku 40 bila chakula.

Murtala Muhammad Gusau, Imamu wa msikiti wa Ijumaa huko Okenen, katika jimbo la Kogi nchini Nigeria, na mkuu wa kituo cha kueneza Uislamu alisema katika mahojiano na BBC kwamba kulikuwa tofauti nyingi kati ya Waislamu na wasio Waislamu katika kufunga.

Kufunga ni njia nyengine ya kumuabudu Mungu kupitia kutokula, kunywa na kufanya tendo la ndoa, kutoka alfajiri hadi jioni jua linapotoweka.

Kila mwaka wakati wa mwezi wa Ramadhan Waislamu kote duniani hufunga siku 29 au 30 hali ambayo ni tofauti na ile ya Wakristo na Wayahudi ambao hufunga kwa siku 40.

Aliongezea: lakini wote lengo la ni moja kulingana na amri za Mungu kwa lengo la kusahihisha tabia ya jamii na kuwakumbusha Waislamu kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Sheikh Ibrahim Adamu Disina , kiongozi maarufu wa dini katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Bauchi aliambia BBC kwamba Waislamu hufunga kuanzia alfajiri hadi jioni bila kula , kunywa kushiriki katika tendo la ndoa.

Hatahivyo kuna tofauti jinsi waumini wa dini hizo mbili wanavyotekeleza amri hiyo ya Mungu.

“wakristo hufunga kwa kujizuia kula vyakula fulani , alisema. Murtala aliongezea kwamba Wakristo hufunga kila mwaka lakini kama Uislamu unavyoamrisha ni wajibu wa kila mtu mzima kufunga.

Wayahudi pia hufunga

Murtala Muhammad anaelezea kwamba mbali na Wakristo, waumini wa dini ya Judaism pia nao hushiriki katika kufunga sawa na vile Wakristo wanavyofunga.

”Kama jinsi Waislamu na Wakristo wanavyofunga , pia waumini wa Judaism pia nao hufunga wakimkumbuka mtume Musa alipokwenda mlimani kuchukua amri kumi za Mungu’,’alisema.

“Lengo ikiwa kuzuia kufanya maovu miongoni mwa waumini wake”.

Kufunga miongoni mwa Wakristo

Kuhusu kufunga miongoni mwa Wakristo Mchungaji Joseph John Hayab, Rais wa muungano wa waumini wa Kikristo nchini Nigeria , tawi la Katsina aliambia BBC kwamba biblia inawafunza Wakristo kufunga.

Pia alisema kwamba Yesu Kristo ambaye ndiye mwanzilishi wa dini hiyo pia alifunga ikimaanisha kwamba iwapo kuna tatizo linalomsumbua mtu ama jamii suluhu ni kufunga na kufanya maombi.

Tofauti kati ya kufunga miongoni mwa wakristo na dini nyengine ni kwamba tunafunga kila siku ili kuwa na nguvu katika kutafuta baraka za Mungu katika maisha yetu.

Hatuna wakati fulani wa kufunga, ikilinganishwa na Waislamu wakati wa mwezi wa Ramadan, alisema mchungaji John.

Aliongezea kwamba kuna wakati ambapo baadhi ya Wakristo hufunga siku 40 kwa jina ‘lent’ ambayo tofauti na Ramadhan sio lazima kufunga.

Kulingana na waumini wa dini ya Kikristo, Mtu hufunga kulingana na mipango yake na sio kama Waislamu ambao hula daku alfajiri na kula Iftar jioni.

”Naweza kusema kwamba Wakristo wengi hawafungi funga ya ‘Lent’, lakini waumini wakatoliki na Waanglikana na wengine hufunga kipindi hicho”.

Kulingana na mwalimu mmoja wa Kikristo, waumini wa dini hiyo hufunga iwapo wanahitaji kitu kama vile kuimarisha maisha ya familia, kuimarisha Afya, ama kutafuta kinga kutoka kwa majanga pamoja na mahitaji mengine ya maisha.

Tofauti sita zilizopo kati ya funga ya Waislamu na ile ya Wakristo

•Waislamu hufunga kwa kutumia kuonekana kwa mwezi lakini Wakristo uhesabu mwaka wa Lunar.

•Waislamu hufunga wakati wa Ramadhan kila mwaka huku Wakristo wakifunga mwezi Aprili na siku 10 za Mwezi Mei kila mwaka.

•Waislamu hufunga siku 29 au 30 , lakini Wakristo hufunga siku 40 .

•Katika Uislamu kufunga ni lazima kwa mtu mzima mwenye afya njema na kutofanya hivyo ni kinyume na dini ya Kiislamu lakini katika Ukristo kufunga ni ishara ya kuwa mtu mwema na kwamba haukiuki mahitaji ya dini hiyo unapokataa kufunga

•Kufunga miongoni mwa Waislamu kunaanza alfajiri na kuendelea hadi jioni huku Wakristo funga yao ikianza usiku muda tu mtu anapolala.

•Katika Ukristo inaelezewa kwamba mtumwa anapaswa kuficha kwamba anafunga hata kwa familia yake lakini upande wa Waislamu kufunga ni ibada inayotangazwa na kiongozi wa Kiislamu inapoanza na kukamilika.

Chanzo: BBC

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

TRENDING

To Top