Connect with us

TEMITOPE BALOGUN JOSHUA, (TB Joshua) AFARIKI DUNIA.

TEMITOPE BALOGUN JOSHUA, (TB Joshua) AFARIKI DUNIA.

Top Stories

TEMITOPE BALOGUN JOSHUA, (TB Joshua) AFARIKI DUNIA.

Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua, maarufu kama TB Joshua amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 57.

Kwa mujibu wa huduma ya TB Joshua Ministries, Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 57 alikufa huko mjini Lagos, Nigeria Jumamosi jioni muda mfupi baada ya kumaliza programu za kihuduma kanisani kwake Synagogue Church of All Nation (SCOAN).

“Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua kwenda naye nyumbani – kama inavyopaswa kuwa kwa mapenzi ya Mungu. nyakati zake za mwisho hapa duniani zilitumika katika kumtumikia Mungu. Hiki ndicho alichozaliwa kwayo, aliishi na alikifia,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

TB Joshua Ni mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nation (SCOAN) na Kituo cha Televisheni cha Emmanuel.

Mungu aiweke Roho ya mtumishi wake mahali inapostahili, AMEN.

Chanzo: Jamii Forum, TUKO

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

TRENDING

To Top