Mafundisho

Tembea na Wenye Hekima Somo Kutoka kwa Milca Kakete: Tafakari Mali yako inatumikaje?

Kupitia GospoMedia.com, Mwimbaji Milca Kakete anakuletea kipengele chake maalumu kabisa kinachokwenda kwa jina la Tembea na Wenye Hekima kitachokuwa kinakujia mara kwa mara kupitia tovuti yako pendwa ya GospoMedia.Com.

Leo ikiwa ni sehemu ya kwanza ,mwimbaji Milca Kakete ametuletea ujumbe unaosema “Tafakari Mali yako inatumikaje?” kama ifuatavyo..

“Yawezekana ukimuomba Mungu akubariki na amekubariki ila yawezekana kabisa kwamba kwakuwa hicho alichokubariki nacho hukioni unashindwa kuzihesabu baraka zake sawasawa na mpango wa Mungu. Huenda pia baraka hiyo imekuja na unashindwa kutumia hekima jinsi ya kuitumia kwa mpango wa Mungu. Mfano Matumizi yako makubwa kwa mwezi yanaenda wapi? Unatumia zaidi kwa matumizi binafsi kupita kiasi kufikia mahali kwamba hata hukumbuki “dini iliyo njema” kama Biblia isemavyo? Umewasahau hata maskini,wajane na yatima waliokuzunguka? Mungu asema leo tafakari mali yako inatumikaje! “

MILCA KAKETE ambaye kwasasa anaishi nchini marekani, ila kwasasa anatamba na video ya wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la NATAKA NIKUABUDU ikiwa ni moja ya wimbo uliobeba jina la Album yake mpya iliyo katika mfumo wa DVD inayotambulika kwa jina la NATAKA NIKUABUDU.

Kama hujapata nafasi ya kuitazama video hii mpya ya Nataka Nikuabudu unaweza kuitazama hapa kisha washirikishe na wengine ili nao waweze kubarikiwa.

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Milca Kakete kupitia
Simu/WhatsApp: +1(905)3415664
Facebook: Milca Kakete
Instagram: @milcakakete
Twitter: milca kakete
Facebook Page: Milca Kakete Ministry
Email: milcakakete@yahoo.com

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Xclusive Chat with Kraist Kid: Kuhusu kuchaguliwa kwenye kwenye tuzo za Xtreem na Jinsi ya kumpigia kura.

Next post

Mpigie kura Angel Benard kwenye Tuzo za Xtreem.Maelekezo yako hapa..