Ndoa na Familia

Teknolojia: Mamba kutumika kulinda wafungwa hatari Indonesia

Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.

Budi Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye kisiwa na kizingirwe na mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda wanadamu, kwani hawawezi kuhongwa.

Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo kutafuta mamba wakali zaidi.

Indonesia ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu hiyo kwa miaka mine 2013.

“Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo.

“Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi waruhusu washukiwa watoroke.”

Mpango huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo nab ado haijaamuliwa gereza hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa, shirika la habari la AFP limesema.

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

COMING SOON!! ONE HOPE PROJECT MUSIC ALBUM

Next post

VITENDO VIOVU NI DALILI ZA MWANZO ZA MATATIZO YA AKILI