Video

Tazama Video | Sikiliza & Download Music: Lydia Charles – Twakuabudu

Kutoka jijini Mwanza Tanzania, leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea video mpya iitwayo Twakuabudu kutoka kwa muimbaji wa nyimbo Injili anayefahamika kwa jina la Lydia Charles video hii imeongozwa na studio ya HM production na audio ikiwa imetengenezwa na producer Paul Nguza anayepatikana jijini Mwanza.

Akiongea na gospomedia.com muimbaji Lydia Charles amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kukamilisha albamu yake mpya iliyo kwenye mfumo wa audio(Audio Cd) pamoja na video (DVD) pia anatafuta wasambazaji wa albamu hii iliyobeba jina la Twakuabudu yenye mkusanyiko wa nyimbo 7 zikiwemo Jina lako, Uniongoze Yesu, Tawala, Alipo Bwana, Uhimidiwe na hakuna kama wewe.

gospomedia.com inakukaribisha kuitazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu mpya uitwao Twakuabudu kutoka kwa muimbaji Lydia Charles kisha washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili Baraka hizi ziweze kuwafikia watu wengi zaidi mahala pote duniani na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi au huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Lydia Charles kupitia.
Simu/WhatsApp: +255 759 048 620
Facebook: Lydia Charles
Instagram: @lydiacharles1
Twitter: lydiacharjoy
Youtube: Lydia Charles 

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Stanley Qamara - Kilicho Bora

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Gospel Music Audio: Pitson - Nisaidie