Video

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Fay Destiny Feat Shirlena Hucks a.k.a Malaika – Hold On / Subiri

Tasnia yetu ya muziki wa injili inazidi kukua kwa kasi, na tunayaona matumaini mazuri ya siku za mbeleni kuweza kuwa kitu cha kawaida kwa waimbaji wetu wa hapa nchini kuwa wanasikika sana kwenye nchi nyingine barani Africa, na hata nje ya bara letu. Hata hivyo kuna baadhi ya Watanzania wenzetu ambao tayari wanaishi nje ya nchi na baadhi yao wapo watumishi ambao wanafanya huduma zao huko huko walipo. Gospomedia inafanya jitihada za kuweza kuwasiliana nao ili kupata mawazo yao, na kushauriana jinsi gani ya kuupenyeza muziki wetu wa injili huko waliko, na kupata mtazamo wao wa kuhusu muziki wa injili wa hapa kwetu kuulinganisha na ule wan nchi zilizoendelea.
Kati ya Watanzania wanaoishi nchini Marekani, mmoja wao ni mwanadada Fay Destiny, ambaye ana huduma yake ya uimbaji huko kwenye jiji la Columbus, lililoko kwenye jimbo la Ohio. Fay, ambaye Gospomedia ina uhakika kwamba watu wengi hawamfahamu, ni mtumishi ambaye alizaliwa na kukulia kwenye familia ya kiislamu, na akaguswa na Bwana Yesu, na kuokoka na kuamua kumtumikia Yesu. Gospomedia bado inaendelea na mahojiano na mtumishi huyu na tutakapokamilisha mahojiano hayo tutakuletea yote kwa ukamilifu.
Kwa sasa tungependa kuutambulisha wimbo wake mpya ambao ametoa video hii wiki hii ya wimbo wake unaoitwa “HOLD ON / SUBIRI” ulioimbwa kwa lugha zote za Kiswahili na Kiingereza, na amemshirikisha muimbaji mwingine Mmarekani mweusi anayeitwa Shirlena Hucks a.k.a “Malaika”. Ukiusikiliza wimbo huu, utabarikiwa na sauti yake nzuri na kuamini kwamba kweli kuna vipaji vingine vya kikwetu vilivyoko nje ya nchi ambavyo vikiendelezwa basi itakuwa ni jambo zuri kwa nchi yetu, kwa tasnia yetu ya muziki wa injili Tanzania. Video hii imetengenezwa na si mwingine bali ni Director wetu anayeishi huko Marekani, bwana Alex Joseck, ambaye yeye jina lake sio geni sana kwa wengi hapa nchini kwani ameshawahi kuja hapa nchini mara kadhaa na kufanya kazi na waimbaji wetu hapa ikiwemo Miriam Lukindo Mauki, Jessica BM, Lilian Mariki, Neema Ng’asha na wengineo.
Video hii inapendeza sana na ina story line inayogusa sana kulingana na maneno ya kutia moyo ya wimbo huu. Uangalie na ubarikiwe na Bwana.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kutazama, kusikiliza na kuupakua wimbo huu kisha washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuisambaza Injili kwa watu wengi zaidi wapate kubarikiwa na kuinuliwa kiroho kupitia wimbo huu wa Subiri(Hold On) kutoka kwa muimbaji Fay Destiny na hakika utabarikiwa sana. Karibu!!

Download

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Edgar Mbilinyi Feat Trifaina - Msaada Ni Yeye

Next post

Tazama Music Video: Agatha Mhina - Mkono wa Bwana