Video

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Agness Nkugwe – AchaNikuimbie

Kutoka jijini Mwanza, Tanzania leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea video mpya iitwayo Acha Nikuimbie kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka jijini humo anayefahamika kwa jina la Agness Nkugwe video hii imeongozwa na director Vipper kutoka studio ya cne-tography zilizopo jijini Mwanza. 

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Agness Nkugwe amesema kuwa video hii itapatikana kwenye album yake inayojulikana kwa jina la Tutamuona Bwana ikiwa kwenye mfumo wa DVD ambayo ipo mbioni kukamilika na kuingia sokoni baada ya kuizindua rasmi kwa tarehe ambayo ataitaja hapo baadae mapema mwaka huu.

Akiongeza mwimbaji Agness amesema kuwa Audio CD ya album hii tayari ipo sokoni kupitia maduka mbalimbali ya wasambazaji wa kazi za muziki wa Injili nchini kote hivyo amewasihi wadau na mashabiki zake wote wandelee kumsapoti kwa kununua album hiyo huku wakiendelea kuisubiri DVD yake mpya ambayo anaamini itakuwa ni ya baraka kwa watu wengi sana kwakuwa imeandaliwa kutengenezwa kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu ili kuweza kumbariki kila mtu ambaye atafanikiwa kuipata album hiyo lengo likiwa ni kuisogeza Injili na huduma yake ya uimbaji kwa watu wengi zaidi mahali pote duniani kupitia kazi zake ambazo ataendelea kuziachia na kuzitambulisha mwaka huu kupitia vituo mbalimbali vya radio na televisheni, mitandao ya kijamii na blogs mbalimbali ikiwemo gospomedia.com.

Kama hujawahi kusikiliza wimbo huu, gospomedia.com tumekuwekea wimbo huu wa Acha Nikuimbie uweze kusikiliza na kupakua kisha washirikishe na wengine zaid ili nao wapate kubarikiwa zaidi kupitia wimbo huu kutoka kwa mwimbaji Agness Nkugwe na hakika utabarikiwa sana. Karibu!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Agness Nkugwe kupitia
Simu/WhatsApp: +255 755 562 244/+255658605732
Facebook: Agness Nkugwe
Instagram: @agnessnkugwe
YouTube: Agness Nkugwe

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: David Cosmas - Nioneshe Njia

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Paul Clement - Wimbo