Connect with us

Tazama Video | Sikiliza & Download Audio: Amani Kiwale Feat Naomi Kaduma-Namfurahia Mungu

Muziki

Tazama Video | Sikiliza & Download Audio: Amani Kiwale Feat Naomi Kaduma-Namfurahia Mungu

Kutoka mjini mafinga mkoa wa Iringa, Tanzania. leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tumekuletea video mpya kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayejulikana  kwa jina la Amani Kiwale akiwa amemshirikisha muimbaji Naomi Kaduma video ya wimbo huu inaitwa Namfurahia Mungu ikiwa imeongozwa na director Debro Gabriel kutoka studio za Eagle View pro audio ya wimbo huu ikiwa imetengenezwa na producer Jonas kutoka studio za Rocksound.

Akiongea na gospomedia.com Amani Kiwale amesema kuwa wimbo huu ndio kazi pekee inayobeba jina la album yake ya kwanza inayotambulika kwa jina hilo la Namfurahia Mungu ambayo mpaka sasa ipo tayari na kwa yeyote anayehitaji kuipata yupo tayari kumfikishia nakala ya album hiyo ambayo anaamini imejaa upako wa kiroho na itakwenda kumuinua kwa kila atakayeipata na kuisikiliza, pia Amani Kiwale amesisitiza kwa kuomba sapoti kwa wapenzi wote wa nyimbo za Injili kuendelea kufuatilia kazi zake na habari zake ambazo zinahusu huduma ya Mungu juu ya watu wake ambao ameitwa kuwahudumia.

gospomedia.com tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uweze kuitazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu kisha washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuisambaza Injili kwa watu wengi zaidi wapate kubarikiwa na kuinuliwa kiroho kupitia wimbo huu wa Namfurahia Mungu kutoka kwa muimbaji  Amani Kiwale na hakika utabarikiwa sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma za mialiko wasiliana na muimbaji Amani Kiwale kupitia
Simu/WhatsApp: +255 755 521 070
Facebook: Amani Kiwale
Instagram: @amanikiwale

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

To Top