Video

Tazama Video | Download Music: Florence Andenyi Feat. Martha Mwaipaja – Funguo

Kutoka jijini Nairobi kenya leo tumekusogezea kwako video mpya iitwayo Funguo kutoka kwa mmoja wa waimbaji wenye kipawa cha pekee cha uimbaji wa nyimbo za Injili anayejulikana kwa jina la Florence Andenyi hapa akiwa amemshirikisha mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Afrika mashariki na kati mtumishi Martha Mwaipaja, video ikiwa imeongozwa na director Source kutoka studio za M-Town Production na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Nairobi Records chini ya mikono ya prodyuza Paulo akishirikiana na prodyuza Teddy B.

Funguo ni wimbo unaozungumzia maombi ya Kibali mbele za Mungu, kupitia wimbo huu mwimbaji Florence Andenyi ametumia lugha ya picha kufikisha ujumbe wa kiroho kwa watu wa Mungu ambao wengi wanakutana bna vikwazo vingi ambavyo vinasababisha kutofikia matarajio yao na kupelekea hata kukata tamaa lakini kupitia wimbo huu Florence na Martha Mwaipaja wanatupatia tumaini la kushinda vikwazo na magumu tunayopitia kwa kutusisitiza kurudi na kuwa karibu na Mungu ili aweze kutupatia kibali ya mambo tunayohitaji katika maisha yetu wewe unayehitaji maisha mazuri, wewe unayehitaji mtoto, wewe unayehitaji kufanikiwa kimasomo na wengine wote mnahitaji mafanikio katika mambo mbalimbali tunahitaji kuomba funguo ya kibali kwa Mungu ili tuweze kufika tunapotaka maana bila yeye sisi hatuwezi.

Kwa moyo wa unyenyekevu tunakukaribisha kutazama video hii na kuapakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana na Mungu atakutendea jambo kuu kupitia wimbo huu. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Florence Andenyi kupitia:
Facebook: Florence Andenyi
Instagram: @florencendenyi
Twitter: @andenyiflorence

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mwimbaji Anna Mapessa Kuachia Wimbo Wake Mpya Tarehe 15 Septemba 2017

Next post

Download Official Music: Rehema Lupilya - Mwema