Connect with us

Tazama Video | Download Music Audio: Ritha Komba – Kivulini

Muziki

Tazama Video | Download Music Audio: Ritha Komba – Kivulini

Kutoka jijini Dar es salaam, Tanzania. leo kupitia tovuti yako pendwa gospomedia.com tumekuwekea video ya wimbo mpya kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili anayekuja kwa kasi nchini akifahamika kwa jina la Ritha Komba video ya wimbo huu inaitwa Kivulini ikiwa imeongozwa na Director Mahiri wa video za muziki wa Injili anayetambulika kwa jina la Einxer na audio ya wimbo huu ikiwa imetayaarishwa na producer Kingson kutoka studio ya Mefo Music jijini Mbeya.

Akiongea na wanahabari wa gospomedia.com mwimbaji Ritha Komba amesema kuwa kwasasa anajipanga vyema kuboresha huduma yake ya kimuziki ili aweze kufika kimataifa zaidi ambapo kwasasa yupo mbioni kuzindua rasmi studio yake mpya ya muziki ambayo itakuwa inamrahisishia kazi zake za kimuziki na kuwasaidia waimbaji wengine ambao watahitaji huduma hiyo mbali na kuzindua studio yake ya muziki pia anatarajia kufanya tamasha kubwa linaloitwa Mwanamke wa Imani litakalofanyika tarehe 17.09.2017 lengo la tamasha hilo likiwa ni kuwakomboa mabinti na wanawake kupitia mafunzo na semina maalumu itakayosindikizwa na burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

gospomedia.com inakukaribisha kwa moyo mkunjufu kabisa uweze kuitazama video hii ya Kivulini, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao na hakika utakuwa baraka katika maisha yako kuanzia sasa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ritha Komba kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook:
Ritha Komba
Instagram:
@rithakomba
Email:
rithakomba@yahoo.com au synyoritha@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top