Video

Tazama Video | Download Music Audio: Genecic Various Artist – Mfariji wa Kweli

Katika muendelezo wa maombolezo wa msiba wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea video nyingine ya wimbo wa maombolezo ya ajali ya wanafunzi waliopoteza maisha wakiwa kwenye basi huko mkoani arusha wimbo huu unaitwa Mfariji wa Kweli kutoka kwa kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Arusha lililo chini ya Management ya kampuni ya Genecic ambayo inajihusisha na kusimamia kazi za wasanii muziki hasa wa muziki wa Injili huko mkoani Arusha wimbo Huu umefanyika ndani ya studio ya Genecis na video ikiwa imefanywa na studio hiyo pia.

Ikumbukwe kuwa msiba huu umehusisha wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent ambao walipata ajali ya basi iliyotokea katika korongo la mlima wa Rhotia, karatu, mkoani Arusha siku ya jumamosi ya tarehe 6.05.2017 ambapo imethibitishwa kuwa zaidi ya wanafunzi 25, walimu wawili na dereva mmoja wa basi la shule ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha wamefariki dunia wakiwa ndani ya basi hilo ambalo lilipata ajali.

gospomedia.com tunakukaribisha uweze kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu wa majonzi na salamu za rambirambi kwa wafiwa wote ambao wamefikwa na msiba huu mzito.

Download

Uongozi na timu nzima ya gospomedia tunapenda kuchukua nafasi hii pia kutoa pole kwa wafiwa wote na taifa kwa ujumla, tunazidi kuwaombea kwa Mungu azidi kuwatia nguvu ya misuli ya imani katika kipindi hiki kigumu ambacho tunaamini Mungu atakwenda kuwasimamia, “Bwana Ametoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe”.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: Nassoro Mnyali - Kwake Yeye

Next post

Habari Picha za Uzinduzi wa Album ya Nimegusa Vazi Ya Witness Mbise Ndani ya Kanisa la CAG Ubungo